Niamini Lyrics
- Genre:Bongo Flava
- Year of Release:2001
Lyrics
Niamini - Professor Jay
...
*Niamini sema nataka uwe na mimi, mama
Watu wenye fitina wanaleta majungu uachane na mimi, eeh
Hivi kwanini sema hutaki kuniamini mama, nyayo ziko pamoja mpaka siku ya kifo, uanze wewe au mimi*2
Nakupenda sana ingawa wanakuita demu wa uswazini,penzi lako la kweli ndo kitu nachothamini kipepeo cha moyo, we sema unachotaka.
Jinsi unavyoenzi kipenzi sina mashaka tulipanda milima tukaja kwenye mabonde,
Na sasa ni tambarare, tufanye wanga wakonde kwani tunapopita wamemwagia mbigili njoo nikumbatie, tufe tukiwa wawili.
Ushangae tukigombana tu wanafurahi, na tukiwa pamoja wanashindwa kutusabahi.
Walishakuja kwangu kunipa habari zako, nikawatoa mbio kulinda heshima yako.
Kwangu wamenishindwa wamegeuza kibao, changanua mapema upime akili zao.
Ni maisha yo Liz, twende tujikongoje,
maisha safari ndefu sijui mbele kukoje.
Wanasema mi nakunywa wee nalala kwenye bar, wanasema mimi ni bingwa la ngono kwenye mitaa, wanasema mimi nimeshawataka wamekataa.
Kwako napiga goti twende kisupastaa
*Niamini sema nataka uwe na mimi, mama
Watu wenye fitina wanaleta majungu uachane na mimi, eeh
Hivi kwanini sema hutaki kuniamini mama, nyayo ziko pamoja mpaka siku ya kifo, uanze wewe au mimi*2