
Hands Up ft. G-Nako Lyrics
- Genre:Bongo Flava
- Year of Release:2021
Lyrics
Hands Up ft. G-Nako - Professor Jay
...
Mikumi stand up
(Tongo records)
Heshimu nguvu ya mashabiki
sio nguvu ya Kiki
muombeni Sana mungu na kupata ni ridhiki
Unasubiri bakuche na kwao jogoo hawiki
Bora sisi tumezoea ugali na sukuma week
Naipinga dhiki na haki haikamatiki
huu no mrima wa baberi na kamwe hautikisiki
Tumetoka mbali na tunapokwenda mbali
Maji kupwa maji kujaa ndio mtindo wa Bahar
Ni king ndani ya jungle
Hip-hop ndio mpango
Tunafanya mambo
Akili mgando tunawaweka kando
Nawapeleka jandoo
Nawachqnganya Kama chanjo
Mc's majigambo migambo nawafanya chambo
Nikikaakaa
Aman kwa Jose mtambo
True niggar in the game kinara toka kitambo
Unawasifu Wana mbio nisifu ninaye wakimbiza
Wanaichafua Sanaa inanuka mayai vinza mmmmmh
uwawawawawa*wawawawwawawa
Mikono juu mwendo wa mateka stop
Kama Kijiji kinazeeka stop
Tumefika wachana mikeka
yule yule ni Jay na Jay ni yule yule
uwawawawawa*wawawawwawawa
niliwaachia waseme hawasemi
Niliwaachia minazi hawagemi
Mikono na ubrother men
Wameufanya mziki unadeni
hawajui tafsida na maadili na tamathali za semi
Hawana wanachofanya wamebaki kulalama na
Kila kunapo kucha wanawaza kulalama
hatuwezi kutazama kizazi kimejaa laana
wale mazee wa mapambio wanaota uteuzi wa mama
Haram inakuwa halali na halali inakuwa Haram
Nakupa hip Hop elim kwa kutumia kalam
Misimamo mwanzo mwisho na bendera inapepea
ninapo anguka nainuka najikunguta natembea
Usiniletee mazonge mm ni Jay wa mitulinga
ukiniangalia kwa jealous unaweza kusema naringa
Unawasifu Wana mbio nisifu ninaye wakimbiza
Wanaichafua Sanaa inanuka mayai vinza mmmmmh
uwawawawawa*wawawawwawawa stop
Mikono juu mwendo wa mateka stop
Kama Kijiji kinazeeka stop
Tumefika wachana mikeka
yule yule ni Jay na Jay ni yule yule
uwawawawawa*wawawawwawawa stop
Yule yule ni Jay na Jay ni yule yule
added by
Prince wa kigoma