
Mimi Ni Nani Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2024
Lyrics
Mimi Ni Nani - Roma Mkatoliki
...
Tongwe Records
BinLaaden
Mnaikumbuka ajali ya Mv Bukoba
Chanzo ni mimi nikaua watu elfu moja
Hata Nyerere hakufa kwa kansa yadamu
Mnajidanyanganya na wengi hamjanifahamu
Nilimua mwalimu huko uingreza
Mv Spices ile ajali niliitengeza
Na hata Lulu ni bure tu mlinga
Mimi ndie niliemuua marehem Stiven Kanumba
Kuna muda ikigoma,sumu naua kwa kisu
Kipindi nipo Dodoma nilitaka kumuua Lisu
Kila mkoa,kila nchi natembea
Nilienda Afrika Kusini nikamuua Ngwear
Marelia ilimuua Langa si etiee
Kweli hamnijui mimi ndie nilie muua yule mwamba
Lusanga,Muheza Tanga
Mnaikumbuka ile ajali ya Sharo Milionea
Mimi ndie nilipindua ile gari
Na Mkude nikamuacha Zuge
Tanga nikamfata Udeude
South wakesema si uje na huku umuue Ruge
Sikufanya ajizi
Nikafata mchizi
Je?ni nani anaefatia saizi
Mi ni nani?
(izraeli mtoa roho) mi sio izraeli mi ni nani?
~we ni mungu basi~
Mi sio mungu mi ni nani?
#labda mtume au Yesu#
Mi sio hao mi ni nani?
Wee nii ninii nii niii
Je mi ni nani?
"mwenzetu basi we jambazi"
Sio jambazi mi ni nani?
+we ndio kifo mwenyewe wewe+
Mi sio kifo mi ni nani?
*shetani we pepo tokaaaa*
Sio shetani mi ni naniiii?
(vilio)
Hivi mnadhani mi naumia nikiona mnalia
Ama mnadhani nahofia nikiona mna fear
Je mi ni nani au mnadhani mnaweza ni zuia
Haiwezekani nawaambia hadi niimalize Dunia
Sina mipaka ndio maana nikautoa uhai wa mkapa
Na mpaka mkazika sikusita tena kumfata. (MAGU)
Na nilikua na ghadhabu nikaondoka na roho yake
Na nchi nzima ikastaajabu
Dandu
Comlex
Banza
Vivi
Mez B
Jey B
Komba
Jizii
Niliwauwa watanganyika wakalia
Hata Bi Kidude,Maalim Seif wazanzibar waliumia
Mbala Mwezi nilimuaa usiku sana
Sam Wa Ukweli sikutaka kumuua mchana
Kwa mzee majuto sikutaka kutumia bunduki
Wengi hamkumbuki jinsi gani nilimuua Sajuki
Mnasahaau
Ndio maana mnayasingizia maradhi
Eti Corona come on
Mimi ndio nimemuua Kijazi
Na hata ukisema unikwepe njia hii hupiti
Wengi wamenikwepa coco Beach
Nimewaulia Kibiti
Je mi ni nani?
Kiitikio.......
Mnakumbuka vituko vya Masogange wa Belle
Mnakumbuka ajali ya kivuko cha Mv Nyerere
Mi ndie nilimuua yule mrembo
Nikazamisha kile chombo
Ajali Segera Mombo
Ni mimi na sio uongo
Ukweli nakupa
Mi ndie nilie muua Amina Chifupa
Hadi Baharini naibuka
Na ndo Pancho nkamkuta
Nikaondoka na uhai wake
Tena papo hapo
Miezi minne nkamuua Zilla
Na sikuishia hapo
Sichagui jinsia
Uwe shujaa uwe na kasoro
Ndio mana nilamuua C-pwaa hata Maunda Zoro
Uwe viongozi wale wanaopendwa na wengi
Ndio mana nkamuua Lwakatare nikaua na Mengi
Wengine nawaulia hospitali nawaua kinyonge
Mnazisingizia ajali mnasema ni pombe
Sijali mnajichanganya ndio mana nikamuua Kibonde
Mnajidanganya mi naua hata mmeze vidonge
Hua nacheka nikiona mnaisingizia Ngoma
Nasema hamjanijua na bado mtanikoma
Na ili mjue mimi apa noma
Ndio mana 2002 nilimuua Babake Roma
Je mimi ni nani?
Written by SUMA DEE