![Usimsahau Mchizi Ft. Moni](https://source.boomplaymusic.com/group2/M01/1A/DE/rBEeM1tr1XKARnDDAAD90ZAwQB4811.jpg)
Usimsahau Mchizi Ft. Moni Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2017
Lyrics
Usimsahau Mchizi Ft. Moni - Roma Mkatoliki
...
Aah Bin Laden
(Tongwe Records For...... )
Verse 1 (Moni Centrozone)
Majengo sokoni wazazi wametulea kwa kuuza gongo,
Ambapo kujiuza na drugs na viinua mgongo,
Maskini vipofu matajiri ni chongo,
Miaka 20 sio percent nishatishiwa na maisha bongo,
(Ndo mana) sichange sura kwa upasuaji wa plastic,
Moni ni ambiguity kwenye maisha semantic,
Chuki timu pinzani na naishindaga hatrick,
Maisha yetu keshachora kipanya the artist,
Kila kona ya mtaa wamejaa watu na viatu,
Watu hawana kazi na wanapata mahitaji matatu,
Ka uliyoshika ni hayo makuu mbele ni shimo,
Zilimopita nyayo za miguu ya mbele ndimo,
Zilimopita nyayo za miguu ya mbele ndipo,
Ninapopita Moni ili kuyasaka malipo,
Nishajimix kwenye viduka vibanda vya mr two touch,
Sikupata mbuli wala sent ya Hassan mwinyi ruksa,
Chorus
Wanangu wa streetlife (wanangu wa kidato mpaka chuoni)
Streetlife (wanangu wa kidato mpaka chuoni)
Streetlife (wanangu wa kidato mpaka chuoni)
Wanangu wa kidato mpaka chuoniii..
Now and then usimsahau mchizi moni,
Usimsahau mchizi moni,
Now and then usimsahau mchizi moni,
Usimsahau mchizi Moniii,,
Verse 2 (Roma)
I'm Angry give a gun le me kill these cochroach,
Coz I'm angry ok kneel down (gun shot),
Nanasi sio tango kulila inahitaji mpango,
Na ukiwa na mpango wa kando ina mana mkeo hajui mambo,
Ukitaka kumkomoa kahaba utaipasua tu kondom,
Au utamchubua kimahaba ujikomoe kisa nyagi na phantom,
Na utajuta ukisha (mmmmmh) halfu kahaba anaovuta mpunga,
Wala hajali kama mpishi anaesonga ugali wa mfungwa,
Wanaunyea mkono wauza sura Yees siukati nauosha,
Wanakula hadi nyama ya chura ingawa wana rasta ka ngosha,
Inachosha natamani kusema inatorture,
Na nawatorture hadi wasisite kusema me ndo kocha,
Vijana hupasahau nyumbani wakishapagawa na jiji,
Usimkere jirani akikunyima hifadhi ya friji,
Kitaa kimeingia shetani me ustadhi nimetoka hiji,
Nauliza nimuokoe nani kila mwamba anajiona gwiji,
Na anaeithamini tungi Yees ataidharau tochi,
Penati inahitaji ufundi utapaza ukipiga dochi,
Mungu wa Roma note, ndo Mungu wa Bakhresa,
Me nna sijda kwenye goti so don mess up,
Chorus
Wanangu wa streetlife (wanangu wa kitaani mnanisoma)
Streetlife (wanangu wa kitaani mnanisoma)
Streetlife (wanangu wa kitaani mnanisoma)
Wanangu wa kitaani mnanisomaaa..
Now and then usimsahau mchizi Roma,
Usimsahahu mchizi Roma,
Now and then usimsahau mchizi Roma,
Usimsahau mchiziii....
Tongwe Records For.........
@Kanna De Msomally...