
Nitasimama Tena ft. Abiud Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2024
Lyrics
Nitasimama Tena ft. Abiud - Roma Mkatoliki
...
Yiih
eeeeeh
You ready
Nigongee nchumari men
Nitasimama tena x2
Na imani na imani
Bin laden
Unazaliwa kwenye familia duni ya kifukara
Nyumbani hali mbaya kiuchumi msosi wa duara
Ugali size ya ngumu na mpo saba hamjala
Hata kipande cha sabuni kumudu usifanye masihara
Sayansi ya Mungu utaikufuru kisa njaa
Maana huwezi chagua aina ya mzazi ataekuzaa
Jirani kazaliwa na waziri wewe mama yako kichaa
Baba mlevi alafu konda tu wa daladala kibaha
Daah usikate tamaa unamute snea upate hamasa
Wewe ndo wakuibadili sura ya familia kuanzia sasa na unaweza mbona wameweza waliotangulia na wanakichwa kama wewe
Na hawana mkono wa bandia
Pia sikia mzazi maisha haya usichague kazi
Na nikuweke wazi usisikilize watakao kujaji
Kuna wadada baadhi wanaamini wana wanahadhi
Hawaani hawakazi na wala nini hawawazi
Daah non sense born poor die poor no offense
Wacha niwajuze msichokijua
Tuna akili zaidi yenu ila mnanguvu zaidi yetu
Na nguvu ni mtaji wa akili hadi apo hamjaliona gap???!
Sasa mnakwapa wapi ingia mzigoni amka dada
Maisha haya usimtegemee ndugu atakupa msaada
Tafuta chako haina furaha iyo hela ya manyanyaso na kuna raha kula pesa uliyoitolea jasho
Nitasimama tena x2
Na imani na imani
Utasimama tena X2
Na imani na imani
Kuna muda unapamba na kila dili linajamba
Na unakutana na miamba inachana misamba dahw
Mungu mimi nakosea wapi relax hizi ridhiki amezipanga kwa namba
Yako itafika na am sure he never lie
God is awesome faith forever die
Hurt for the passion for the possible you know why
Make impossible,possible easy …….can ….
Na cycle kwenye maisha ndo kitu ambacho
Tuoneshe marafiki zako tukuambie tabia yako
Marafiki wana nafasi ya kubomoa au kukujenga
Ka kamasi eitha ulirushe ndani kama hutaki penga
Ukipata usiwasahau ukikosa watakudharau
Imekaa kimtego ishi nao kiakili wadau
Maana mjini pagumu ila pazuri ukiwa na cash
Ukipata tumia kwa akili tushawazika wengi kwa stress
Na maisha sometimes yanayumba mjini tunateseka unatamani urudi home unawaza mdogo watancheka
Unaona no sweat muhuni acha nikomae sikuwa commited, expection ikishindwana na …. Unakuwa …..
Ukifeli mjini home ukaweke kambi
Rudisha mpira kwa kipa kuanza upya sio dhambi
Wasikilize wazazi changanya na zako
Rudi mashambulizi yoh the man na hiyo nd hustle
Rule number one familia kwanza wekeza kwa watoto
Na sio bar huo ni ushamba
Jipige kifuani mara tatu wewe ni mjanja ukianguka simama tena anza anzaa
tasimama tena x2
Na imani na imani
Utasimama tena X2
Na imani na imani
tasimama tena x2
Na imani na imani
Utasimama tena X2
Na imani na imani
Bin laden “am on Instagram asa G_uniquetz”