Namuachia Mungu ft. Appy Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2024
Lyrics
Namuachia Mungu ft. Appy - Roma Mkatoliki
...
SMG
Instrument
eeh
Sasa hebu mtazame mwanamke mwenzio analia
anamlilia mumeo na upo nae umemfungia
Hii wiki ya pili na hajaiona familia
na kwakua anakuhudumia
basi unayaona umeyapatia
ila naumia ukifikiria izo changamoto
kadi ya benki umeizua na unajua analea watoto
Yani wao waokote kuni we uje tu kuota moto
Unaoufanya ni uhuni na ukahaba wa kitoto
Chozi lake la kilio ni laana ya waziwazi
Mtoto wa mwanamke mwenzio we umeenda kumvunjia nazi
Kama mganga wako mkali angekupa wako akuhifadhi
ukisemwa unajiko kali tusikukaushe kizazi
My dear malipo ni hapahapa kwa dunia
Kama sio kwako hata kwa mtoto na hata kama hana hatia
Sasa kwanini hutaki mwachia mme wa mtu sumu nakwambia nakuhusia unajihukumu utajilaumu na utaumia
Umemchanganya umenda kwa waganga
Mpaka nyumbani kwangu kaondoka
Kisa akuhonge wewe akutunze wewe
Watoto wanateseka
Utamu umezidisha dawa amekuwa mjinga umemfanya zezeta
Heshima ya mwanamke ni ndoa majirani wananicheka yehyehyehyaiehh
Mi namuachia Mungu “Mungu wangu hajawahi kushindwa”
Mi namuachia Mungu yeeih yeeeh
Mi namuachia Mungu
Mi namuachia Mungu
Hakuna tuzo ya ushindi kwa kuvunja ndoa za watu
Yani mwenzio ashindie magimbi na unajua ana watoto watatu
Nakushangaa unafuraha mtoto wa mwenzio analala njaa
Na unapata usingizi juu ya kifua cha huyo jamaa
Na unashare huoni kinyaa kifua changu hakina friji
Leo nautangazia mtaa mwana umerogea rufiji
Na utamba unajiona gwiji
Kumbe mshamba tu wa hili jiji
Unadanga tamaa imezidi na hata sanda tunakuahidi
Hakuna marefu yasiyo na mwisho we endelea tu kujiona mafia
Mwenzio anafunga novena mtakatifu rita karshia
Na haiongopi ile katu
Itamjibu itamtolea hizi tabu
Umenunuliwa macho matatu
Mwenzio ana kiswaswadu
Nafsi yake inavyoumia itakutesa hadi kizazi
Unashare na huyo baharia mweshio uwaletee maradhi
Non fair mfungulie mshikaji arudi kwake
Familia inamuhitaji please inusuru ndoa yake
Umemchanganya umenda kwa waganga
Mpaka nyumbani kwangu kaondoka
Kisa akuhonge wewe akutunze wewe
Watoto wanateseka
Utamu umezidisha dawa amekuwa mjinga umemfanya zezeta
Heshima ya mwanamke ni ndoa majirani wananicheka yehyehyehyaiehh
Mi namuachia Mungu “Mungu wangu hajawahi kushindwa”
Mi namuachia Mungu yeeih yeeeh
Mi namuachia Mungu
Mi namuachia Mungu
Mie nakesha ninapiga goti
umemuweka kwenye chupa hatoki
Wewe kutwa anakumwagia noti
Watoto wanashindia karoti yeehhhh
Mi namuachia Mungu”Mungu wangu hajawahi kushindwa”
Mi namuachia Mungu yeihyehyeeeh
Mi namuachia Mungu
Mi namuachia Mungu
Yehiiiyeeeeh
Instrument
SMG “am on Instagram as G_uniquetz