Dunia Mapito Lyrics
- Genre:Afrobeats
- Year of Release:2013
Lyrics
Dunia Mapito - Matonya
...
Ahh dunia a
Bado nikiza, bado nikiza
Na marashi ya dunia siyasikii
Najihisi nipo kuzimu naishangaa sayari hii
Iliyojawa wanasiasa, michezo na wasaniiiii
Najiuliza wamekuja huku kutalii
Au wamesha hamia 'Dunia ndo Haijirudii'
Mara nasikia swali kama la nguvu za hoja
Dandu ananiuliza, albamu zinajikongoja?
Vipi mmegonga kopi chini ya milioni moja?
Jibu zinalipa sio moja kwa mojaaaaah
Steve 2K anauliza bifu zinaendeleaa?
Nimesha msamehe Castro ameshatoka Segerea?
Namjibu bifu lipo na vita vinanyongea
Castro bado anaoza, tuanzeni kumuombea
Complex naye anauliza 'albamu ile ya Wagosi
Walishagonga kopi ngapi hadi sasa kwa wadosi?
Namjibu tangu ufe mambo yote ni mikosi
Makundi yanavunjika duniani tunakumiss
Yea yie yie
Dunia Mapito jamaa
Tuwaombeeni waliokufa wende salama
Mi nawe tupo, hatujui siku yetu lini
Kinachotakiwa tuishi kwa amani duniani
Yea yie yie
Dunia Mapito jamaa
Tuwaombeeni waliokufa wende salama
Mi nawe tupo, hatujui siku yetu lini
Kinachotakiwa tuishi kwa amani duniani
Kulia nafuta chozi, kushoto lanidondoka
Nakosa raha TX Moshi nikimkumbuka
Muone ananiuliza muziki wa dansi ndio ushashuka?
Jibu bado upo
Ila naamini pengo lako halitozibika
Mara kwambali nasikia sauti ya gitaa
Sauti ya gitaa inapigwa huku inaniita
Kumbe mzee wakale, hayati Bob Marley
Ananiuliza mziki wa reggae unaenda vipi?
Reggae bado ipo
Ziggy na Damian nahisi wanagonga copy
Marijaniiii
Ananiuliza muziki wangu
Unaimbwa sana duniani
Vipi familia yangu Inafaidika kitu gani?
Jibu mimi sina labda mwanao Marijani
Kiza ni kinene sioni pa kupapasa
Mara kwa mbali nawaona wanasiasa
Machozi yananitoka, chini nadondoka
Namuona Karume na Nyerere
Julius wananiuliza 'Muungano je unanafasi'
Nawajibu msiwe na wasi
Sasa Ari mpya, Nguvu mpya pia na Kasi
Ulimwengu mmeuacha dunia ndio inawamissi
Yea yie yie
Dunia Mapito jamaa
Tuwaombeeni waliokufa wende salama
Mi nawe tupo, hatujui siku yetu lini
Kinachotakiwa tuishi kwa amani duniani
Yea yie yie
Dunia Mapito jamaa
Tuwaombeeni waliokufa wende salama
Mi nawe tupo, hatujui siku yetu lini
Kinachotakiwa tuishi kwa amani duniani