Siku 462 ft. Walter Chilambo Lyrics
- Genre:Bongo Flava
- Year of Release:2023
Lyrics
aah aah aaaaah tongo record bin laden
bila mkono wako na neema yako huruma
zako nisinge kuwepo
bila msaada wako ooh woooh
na macho ya ko kunitazama nisingelikuwa hai wooh uwooh ooooh ooohhh aaaah Asante aaah Asante wooh uwoh aah Asante Asante eeh
kweli nimeamini duniani tunapita na akuna wakubisha pale MUNGU anapokuita nilikua kama mfu siku chache zilizo pita Asante sana MUNGU umenipigania hii vita nilikuwa kwenye dhihara tunaita chaka kwa chaka ilikuwa na neema na imejaa baraka tulianzia manyoni mto wa mmbu na babati chato bukoba tarime shirati kakora kagongwa mbalali na kahama tukarudi kigambon I new rasko dar es salaam baaada ya siku chache nikarekea mafinga chunya makambako chombe mpaka mbinga nikaenda mbeya na kumalizia songea ilibidi nikatize dhihara sikuendelea baada ya dhiara ndefu nilijisikia kuchoka ilibidi nirudi home ila uchovu haukutoka jan 24 mwaka 2022 nilijisikia vibaya na kudhohofika mwili mke wangu alinikimbiza hospital ya kitengule baada ya hudama ya kwanza walinikimbiza lugalo hali ilikuwa mbaya wakanipima upesi upesi walinikimbiza muhimbili kwa ambulance ya jeshi nilipofika muhimbili moja kwa moja i.c.u Asante sana MUNGU kila wakati I see you
bila mkono wako na neema yako
huruma zako nisingekuwepo
bila msaada wako ooooh ooh
na macho yako kunitazama nisingelikuwa hai
wooh wooooooh oooooh Asante aah Asante
wooooh Asante Asante
nilipumua kwa machine hali ilikuwa mbaya kila kona ya mwili niliwekewa mawaya moyo wangu ulisimama madaktali walipo sema waliu pampu saa zima ndio ukafanya kazi tena mapafu yalijaa maji na Figo kuwa na mchanga nilishindwa kupumua kabisa na kutangatanga mwili ulikuwa unavimba sababu ya sumu mwilini nikaanza kufanyiwa dayalisisi kutoa sumu mwilini napewa chakula kwa mpira kupitia puani wakawa wanavuta uchafu kupitia mpira kinywani wakasema haisaidii bora wanitoboe koo sauti yangu ndo mtaji ndugu wakasema no uchafu ukaongezeka siwezi ata kukohoa ndugu na madatkari wakakubaliana kunitoboa mana wangenipoteza bila ya uchafu kuutoa baada ya siku chache ndo nikaanza kupumua powa nilikaa i.c.u kwa siku 127 icu pasikie namshukuru MUNGU baba maana saa nilio lazwa nao walipotea namimi nilijua muda wote ntapotea nilipoteza kabisa matumaini ya kuishi muache MUNGU aitwe MUNGU mpaka leo naishi siku moja nilichomoa mipira ya dayalisisi madaktali walishangaa kwani haikuwa rahisi MUNGU ameniponya sijafanyiwa mpka leo hii ni kama movie kwenye banda la video madaktali wanatibu MUNGU Ndie anaponya Asanteni mlio niombea aimeni
bila mkono wako