Kimya Kimya Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2023
Lyrics
Kimya Kimya - Goodluck Gozbert
...
Yeye abomoaye boma
Nyoka atamuuma bwana
Anichimbiaye shimo
Atatumbukia humo
Ahe!! Sababu hii najua mimi napendwa, iyeh!
Tena si wa dunia
Nilishatengwa eeh!
Maagano na Mungu najua eeh!
Shida sio mawingu na mvua eeh!
Akisema nitalima mtaona ninalima
Akisema nitavuna mtaona nikivuna
Sio kosa langu bwana
Mi napendwa na Mungu
Vile unanichukia wanionea bure
Wote alitukufia karibu nawe unywe
Ukitaka kununa
(Nikasirikie kimya kimya)
Kunichimbia shimo
(Utatumbukia humo)
Ehi! Ukitaka kununa
(Nikasirikie kimya kimya)
Kunichimbia shimo
(Utatumbukia humo)
Heh! Ukitaka kununa
(Nikasirikie kimya kimya)
Kunichimbia shimo
(Utatumbukia humo)
....
Dunia Dunia
Inayo mambo aye!
Watu watu
Wanayo mambo aye!
Ukasema ufatilie
Rafiki zako ni adui
Siri wanazoteta nawe sio siri ngoja nikwambie
Si unaona mwenzio
Nikifanikiwa sisemi
Mwendo ni mapambio
Nampamba Mungu mbinguni
Yusufu aliota akasema wakamuuza
Ila ninachojua eeh!
Ya Mungu hayabadilishwi
Sio kosa langu bwana
Mi napendwa na Mungu
Vile unanichukia wanionea bure
Wote alitukufia karibu nawe unywe
Ukitaka kununa
(Nikasirikie kimya kimya)
Kunichimbia shimo
(Utatumbukia humo)
Ehi! Ukitaka kununa
(Nikasirikie kimya kimya)
Kunichimbia shimo
(Utatumbukia humo)
Heh! Ukitaka kununa
(Nikasirikie kimya kimya)
Kunichimbia shimo
(Utatumbukia humo)
Eeh! Ukitaka kununa
(Nikasirikie kimya kimya)
Kunichimbia shimo
(Utatumbukia humo)
....
Enda uliza wale waganga
Kutoka Sumbawanga
Wanajua mimi nalindwa
Nalindwa ninapendwa
Uliza wale wachawi
Kutoka Sumbawanga
Wanajua mimi nalindwa
Nalindwa ninapendwa
Oya! Prokoto bwana mapepo
Umeukanyaga moto, to!
Mimi sio mwenzako
Kacheze makopo, po!
Prokoto bwana mapepo
Umeukanyaga moto, to!
Mimi sio mwenzako
Kacheze makopo, po!
Oya! Prokoto bwana mapepo
Umeukanyaga moto, to!
Mimi sio mwenzako
Kacheze makopo, po!
....
... Asante!!.
Written by Justin.S