![Acha Waambiane](https://source.boomplaymusic.com/group10/M00/01/27/9d04e5ce62bf4c8ba55775dfda5a835f.jpg)
Acha Waambiane Lyrics
- Genre:Afrobeats
- Year of Release:2017
Lyrics
Acha Waambiane - Goodluck Gozbert
...
Acha waambiane wasemezane mabaya yako ila wataambiana wema wa MUNGU maishani mwako
Acha waambiane wasemezane mabaya yako ila wataambiana wema wa MUNGU maishani mwako
Usikate tamaa na yale unayoyaona
ata kama uko chini sanaa( chini sanaaa)
najua wataambiana wewe ni masikini
lakini usichoke ipo siku watasema
najua wataambiana wewe hufai
na umeshatembea na wanaume wengi(tena wengi)
utakapofika wakati wa kuinuliwa aah
utashangaa wakiambiana tena aah( wakiambiana tena)
ati yule mwanamama aliyekuwa ni kahaba (ni kahaba)ameolewa sasa ana familia yake
utaskia tena yule aliyekuwa kikaragosi leo anatembelea gari wataambiana weee
Acha waambiane wasemezane mabaya yako ila wataambiana wema wa MUNGU maishani mwako
Acha waambiane wasemezane mabaya yako ila wataambiana wema wa MUNGU maishani mwako
aaaah eeeh aaaah aaah uuuyeee aaaah eeeh mamaah
Neno hili limekuwa la kawaida kwako (tena sana)lakini lina maana kubwa waweza kuona wanadamu wanatembea kimya kimya ila wametunza mengi mioyoni mwao usije kuona wanacheka na wewe hujui moyoni mwao wameweka niiini waweza ona wanakusalamia kwa furaha zote ila kumbe wameshaambiana ambiana
kwamba yule pale ni mhadhirika wa ukimwi mara yule pale ni mgumba ati yule pale alifeli kidato cha nne na yule pale hana ada ya masomo
(acha waambiane wasemezane mabaya yako)ipo siku wataambiana tena aah vile MUNGU atavyokuinua baba lazima wataambiana tena aaah(ambiana tena aah)
acha waambiane (vile YAHWEH) wasemezane (atavyokuinua juu) mabaya yako lazima mama wataambiana tena
utasikia:;yule mgumba sasa amezaa(ana katoto keupe)aliyefeli siku hizi ana digrii(ana digrii)
utasikia mengiii na utamtukuza MUNGU hivyo usife moyo acha waambiane
(Acha waambiane)
Acha waambiane wasemezane mabaya yako ila wataambiana wema wa MUNGU maishani mwako
Acha waambiane wasemezane mabaya yako ila wataambiana wema wa MUNGU maishani mwako
Acha waambiane wasemezane mabaya yako ila wataambiana wema wa MUNGU maishani mwako eeeh
lyrics by Naom Kerubo AKA Kadot