
Call Za Minuso ft. Franken Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2022
Lyrics
Call Za Minuso ft. Franken - P Mawenge
...
Oyaa Dulla pande zipi.?
Leo Arobaini ya Mzee mrisho na kama unavojua hayakosi madikodiko
Ukichelewa usije Kuta Cha mwisho mwisho
Ukoko kibao huwezi kwangua bila kijiko
Niko na kina Side wakali wa Tongenyama
Sitaki kula nao hawa Wana "Hujasikia habari za kwenye Shughuli ya jana"
Allen kafuta plate sita watu wanatazama
Sahau vyote mwana ila ndizi njoo nayo na Pilipili mbili Gengeni Kwa Mzee Shayo nna mwani wa msosi nshaanza kupiga mwayo
Ila mwana Siri yetu yasiende Milard Ayo
Harakisha mwanang ushafika mda wa mnuso shaba kama zote zinashushwa na Fuso Plate mbili Kila mmoja na mgawaji yupo ila kingi sana Man kama Vipi beba Mifuko
We Usikatae
Call za Minuso
Izi call za minuso (Call za Minuso)
Wee mwana Usikatae (Call za Minuso)
Hizi ndo call za Minuso
Hakuna Mtu mdwanzi asee ka Mzee Khalid yani kwenye misosi huyu Mzee anapenda Ligi
Anapiga matonge kibao lakini hashibi na kapero lake huyo cheki anavokuja Spidi
Kwenye mambo ya misosi huwaga Hana Masihara kwenye Bday za watoto hadi kwenye Vipaimara
Havui Cape mana kichwani bonge la Para
Na Kila akipiga plate moko anashushia Sigara
Sophia Aah sistaduu anatuektia
Kama huamini kutana nae kwenye Sinia
Hanaga pozi mwana jinsi anavoshambulia Kuna siku alipaliwa mpaka akajitapikia Chaji kabisa Simu tusije kulaumiana Kwa kina Ngosha naskia kesho ni Ndizi nyama
Kinaliwa mapema mchana baada ya adhana washashusha mbuzi sita wakubwa kima Cha Ngama
We Usikatae
Call za Minuso
Izi call za minuso (Call za Minuso)
Wee mwana Usikatae (Call za Minuso)
Hizi ndo call za Minuso (Call za minuso)
Hii hapa Hii hapa
Wana wamenipigia Hii hapa
Hii hapa Hii hapa
Call ishaingia Hii apa
(Bingo BEATS)
Hii hapa Hii hapa
Wana wamenipigia Hii hapa
(Lyrics by AT Man Don )