
Customer Care ft. Dj Gold & Foby Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2022
Lyrics
Customer Care ft. Dj Gold & Foby - P Mawenge
...
Juzi tupo zetu dampo niko na wanangu wa bodaboda
Siku ilikuwa ngumu abiria mmoja-mmoja
Nikasema leo ghetto ni ugari na mboga-mboga
Maana mpaka sasa haionekani dalili ya vitoga
Basi nimetulia tu naminya-minya simu
Huku nawaza nani leo nimuharibie stimu
Hata sijui ni wapi mawazo yalipotokea
Eti nijaribu kumtongoza customer care
Basi nikapiga moja zero zero fasta
Na kila nikisikia sauti ya kidume nakata
Nikajaribu kama mara tano hivi sikupata
Kupiga mara ya sita mtoto huyo kanasa
Hello! Habari, unazungumza na happy
Unaitwa nani na unapiga simu toka wapi
Jina langu mawenge naishi kiwarani
Ni bodaboda hapa bomubomu barabarani
Ahaa asante sana kwa kutupigia
Nini tatizo lako tuweze kukuhudumia
Aaaah simu zote nazopiga zinakata
Yaani sijui sababu ni nini mpaka nadata
Kama salio mbona muda wa maongezi ninao
Naomba nichekie labda ni masuala ya mtandao
Okay! Tafadhali nakuomba usubiri
Usikate simu nakushughulikia dk mbili
Aaaah, Kiukweli kabisa nimefurahi ulivyo mkarimu
Unanivutia kwa kukusikia tu kwenye simu
Amini kwamba mwenzako umeshanitia wazimu
Kama upo single naomba hiyo nafasi muhimu
Heee! Aiseee mbona umefika mbali
Unanifahamu kama nimeolewa tayari
Sio mbaya na mimi pia na-test zari
Inaweza kuwa bahati yangu na ukanikubali
Tafadhali sana mawenge usiwe mbishi
ebu kata unajua hii ni simu ya ofisi
Sawa lakini hii mimi ndo namba yangu
So nicheki humu ukitaka kunipa jibu langu
Kupita dk kumi tu ujumbe nikapokea
Save namba yangu mimi ndio yule ccustomer care
Mzee nikaomba date bila kuchelewa
Leo niko naye ghetto na ugari nishasongewa