Neno La Kalvari Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2021
Lyrics
Neno La Kalvari - Ambwene Mwasongwe
...
Nakuhitaji Bwana wangu
Mimi niko wazi
Unisikilize
Kama utapita njia hii
Uje unione
Nikuonyeshe mahali
Panapouma
Moyo wangu
Wanaona shauku
Eee Yesu Bwana wangu
Unirehemu
Mwili wangu unaumwa
Kweli nimechoka
Hata waoaniuguza nao
Wamenichoka
Maisha yangu yamekuwa gharama
Kweli nakuhitaji wewe tu
Usiniache peke yangu
Nitaaibika
Linga kwisa
Gwendepo pamyangu
Nguhelepo simo
Isya munda myangu
Lelo linga kukinda ungikindaga kimyeye
Ujobhe ilisyu limo na une angusangaluka
Tata umbumbulusyege
Umbumbulusyege
Usyele gwimwene
Gwe mmanyani gwani
Linga nakupalaga imbalo
Jesu gwe mmanyani gwangu
Nakukolelaga ingamu jako
Natigi Jo ugwe Mwajesu
Enaa
Usyele gwimwene gwe mmanyani gwangu
Enaa
Usyele gwimwene gwe mmanyani gwangu
/~~~~~~~~~~~~~~~\
\~~~~~~~~~~~~~~~/
Maji yakimwagika
Yasizoleke tena
Nitakufuata wewe
Uwezaye yazoa
Upepo ukinivumia
Na kuniacha sina kitu
Nitakukimbilia wewe
Uwezaye kuushika kwa konzi
Roho ikifa ndani yangu
Nikabaki na mwili wa mnyama
Nitasubiri neema yako
Kisha nitazaliwa upya
Ninaibariki kazi ya msalaba
(Kalvari)
Neno la Kalvari, neno la Kalvari
Limeleta ushindi, neno la Kalvari
Ninalibariki
Jina lako libarikiwe
Baba wewe ni mtoshelevu .Hakuna aliye kama wewe, Ndipo Ayubu akainuka akalirarua joho lake Kisha akanyoa kichwa chake nakuanguka chini
Na kusujudia, akasema mimi nalitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana libarikiwe.
Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi wala hakumwazia Mungu Upumbavu.
Jina lako libarikiwe.