Chozi La Haki Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2021
Lyrics
Chozi La Haki - Ambwene Mwasongwe
...
Bado na kumbuka maono
Niliyoyaona zamani
Nalimwona Bwana ameketi
Amezungukwa na halaiki
Naliona watu makundi makundi
Wakimwendea wapewe haki
Tena nalisikia sauti za vilio
Wakimmiminia machozi miguuni
Nalisikia majina ya watu yakitajwa
Majina ya nchi, majina ya viongozi
Kutoka ardhini misituni na majini
Sauti ya damu ikidai kisasi
Naliona wingu jeusi la laana
Likipafunika kila penye dhuluma
Tena Naliona Malaika wa ole
Akipiga kelele kuwaambia watu
Ole wako wewe utendaye dhuluma
Ole wako wewe uoneaye
Ole wako ghadhabu inakuja
Ole wako ewe nchi ya dhuluma
Ole wako nchi isiyo na haki(Ole wako)
Ole wako watu wangu
Ole wako watu wanaodhulumu
(Ole wako taifa langu, Ole ole)
Ole wako nchi isiyo na haki
(Bwana ana ghadhabu)
Bwana ana hasira
Sababu ya kilio cha mnyonge
Hee Olee,
Ole wako unayefanya hila
Ole wako unayeumiza watu
Ole wako kwa ajili ya damu
Ole wako kwa ajili ya kilio
Jina lako limetajwa
Umeng'ang'aniwa mbele za Mungu
Oleeee! Ole Ole ah!
"" "" "" "" ""
Nalimwona kijana jeuri
Aliyemuumiza mwenzake
Akagoma kumwomba msamaha
Akidhania yuko salama
Naye akasogea kwa Mungu
Tena akapeleka na sadaka
Akamwacha ndugu yake analia
Kamwachia maumivu moyoni
Jina lake likatajwa
Katika waliong'ang'aniwa
Jina lake likadaiwa adhabu
Jina lake likadaiwa hukumu
Yesu akaagiza agizo
Niwaambie watu wake
Warekebishe makosa Yao yote
Kabla hawajalipa senti ya mwisho
Hukumu yake ni kali kuliko radi
Ghadhabu yake inawaka kama moto
Ukitajwa Jina lako utaadhibiwa
Uhakikishe umelipa senti ya mwisho
Patana haraka
(Nakuonya ndugu yangu ) na mshitaki
Patana haraka (Nakushauri leo) na mshitaki
(Patana na watu wote)
Atakufikisha pabaya
(Patana na mme wako, Patana naye)
Kabla hajakufikisha pabaya
Patana haraka (Heeeei)
Na mshitaki
(Nakuonya)
Patana haraka (Nakuonya mama) Na mshitaki
Atakufikisha pabaya
Usije ukalipa hata senti ya mwisho
Kabla hajakufikisha pabaya
(Huko utalipa hata senti ya mwisho)
"" ""
"" ""
Ole wako nchi isiyo na haki(Ole wako)
Ole wako watu wangu
Ole wako watu wanaodhulumu
(Ole wako taifa langu, Ole ole)
Ole wako nchi isiyo na haki
(Bwana ana ghadhabu)
Bwana ana hasira
Sababu ya kilio cha mnyonge
Olee, Heee Olee!
Ole wako unayefanya hila
Ole wako unayeumiza watu
Ole wako kwa ajili ya damu
Ole wako kwa ajili ya kilio
Jina lako limetajwa
Umeng'ang'aniwa mbele za Mungu
Oleeee! Ole Ole ah!
"" "" ""