Nimeachilia Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2023
Lyrics
Nimeachilia - Ambwene Mwasongwe
...
Ulipanda mti mzuri
Ukategemea kuvuna matunda
Ila mti wenyewe,umezaa miiba na michongoma
Uliwekeza muda na mali ukamwagilia ukitarajia matarajio yamekuwa sio sasa umebaki na maumivu
Japokuwa uliiyona miiba ulijipa muda ukapogolea ulitarajia mabadiliko labda kesho mti utazaaa
Sasa imekuwa kinyume mti wako mwenyewe unakuchoma
Unalia (aaaaah)
Ukikumbuka mbegu (aaaaah)
Unalia (aaaaah)
Eeeeh ukikumbuka maji (vumilia)
Unalia (aaaaaah)
Ukikumbuka kazi
Sio kila kinachokuja kwako ni chako
Na sikila kiondokacho kwako ni chako
Hata kama unavipenda sio vyako
Vingine Mungu huviondoa
Ili wewe ubaki salama
Iwe kazi,nafasi,mahusiano au cheo
Japo vyaondoka kwa maumivu
Ila jifunze kuviacha viende
Nafasi ya moyo wako mpe MUNGU
Chochote kile kikuumizacho
Kufikia hatua yakukuua
Jua ulikikalisha mahali pa MUNGU
Jifunze kukiacha kiende
Jifunze kusema bye bye
Maana sio vyote vyakwako
Walitoka kwetu hawakuwa wakwetu
Maana wangekuwa wetu wanglikaa nasi
Walitoka ili wafunuliwe sio wote wakwetu
Walitooka kwetu hawakuwa wakwetu
Wangekuwa wetu wangelikaa nasi
Walifunuliwa ili tujue sio wote wakwetu
Heeee
Nimeachilia jifunzeee kuambia moyo wako (nimeachilia)
Hatakama imeuma sana jifunze kusema (nineachiliaa)
Eeeeh nimesamehe Mungu anaona
Mimi nimeachilia
Tafuta mahali pa peke ako
Mahali hakuna akuonaye
Mahali pa siri pa utulivu
Mahali hakuna akusikiaye
Ukakumbuke machungu yako,maumivu yako
Na machozi yako ukayakumbuke maneno yote
Yakuumizayo moyo wako kakumbuke vitu ulivyopoteza kakumbuke muda na watu wa karibu kakumbuke hasara uliyopata usiyasahau machungu yoyote, pia usibakishee machozi pia usiyameze yoyote toa yanayousibu moyo toa yasibakie yoyote
Aaaah aaaaah aaaaaah
Toa usibaki na machungu
Hakikisha umetuliza moyo
Umesahau yote yaliyopita
Achilia wote ulioshikilia
Waache waende si riziki yako
Hakikisha umekuwa mwepesi
Ji edit moyo ubaki salama
Inuka semaa kwa ujasiri nimeachilia ninaanza upya inuka jikung’ute mavumbi yakale yamepita sasa ni mapya
Nimeachilia, sema nimeachilia
Nimesamehe yote (nimeachilia ,
Nimejinyonyoa manyoya yakale sasa ni mwepesi (nimeachilia) nimeota mapya sasa nipo huru naruka ruka na maisha mapya
Nimeachilia (nimeachilia mimi)
Nipo huru nimejinyonyoa mistawaze nimeachilia
Nimesamehe vitu,muda na wakati niliopoteza
Kwa usalama wa moyo wangu nasema nimeachilia aaaaah ooooh
Nimeachilia
Nimesamehe sasa ninayo amani oooo
Maumivu ya kale nimeacha nyuma
Nimeachilia
Yooo nimefunguliwa
Nimewekwa huru nina amani
Bwana kaniwezesha yooo yoooo sijinyongi tena sijiui tena
Bwana w