Ombi Langu Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2021
Lyrics
Ombi Langu - Ambwene Mwasongwe
...
Huuapia moyo
Nitakulinda
Maana najua kwako
Kuna chemichemi
Nitakujengea boma uwe salama
Adui akija asikuweze
Usiruhusu maneno yakuvuruge
Usiruhusu hasira ikae kwako
Namuweka mlinzi awe ngome yako
Akupiganie ubaki salama
Bwana naomba utete nao
Wale wanaoteta nami
Naomba upigane na adui zangu wote
Mimi sitaki kubishana nao
Sitaki kupambana nao
Nisije nikakosea wakanilaumu
Maana wameshavuta upinde
Wako kwenye mangojeo yao
Wamenuna wamekunja sura
Wana hasira nami
Kinachowafanya wasinidhuru
Ni kwamba hawajapata sababu
Wanahesabu hatua zangu nikosee waninase
Usiache mguu usogezwe
Unaswe kwenye mitego yao
Weka mngojezi kinywani mwangu
Anilinde nisiropoke
"" "" ""
(Heeeeeee)
Hili ni ombi langu kwako
Mungu akukumbuke na wewe
(Akatembee nawe) Akatembee na wewe
(Akatembee na wewe)
Hata uwapo gizani Akulinde
(Moyo wangu) Wewe ni wimbo wangu
(Wewe ni Bwana wangu)
Tena dawa ya moyoni mwangu
(Wewe u fahari yangu) Ufahari yangu
(Wewe ni wimbo wangu)
(Wewe u thamani yangu)
(Wewe u mwaminifu wangu)
(Bwana wewe Unaweza) Aaaaaaa
(Wewe ni Mungu uliye hai) Aaaaaaaa
(Wewe ni mfalme wa ajabu) Aaaaaa
Wewe unayeponya mioyo) Aaaaaaa
(Halleluya)
"" "" "" "" ""
Nifanye kama Yusufu
Uliyemwona mwota ndoto ukambariki
Wewe ulimwona waziri mkuu
Tofauti na wanadamu
Wakamtazama vingine walivyoweza
Baba yake alimwona mpelelezi
Awapeleleze ndugu zake
Ndugu zake walimwona ni mbeya
wakamtupa shimoni
Wamidiani wakamwona biashara
Wakamuuza kwa Potifa
Mkewe Potifa akamtamani
Akamwona kijana mzuri
Wafungwa wenzake wakamsahau
Wakifikiri ni muhalifu
Wewe uliona ndoto ndani yake
Ukamfanya waziri mkuu
Nami nifanye kama Yusufu
Hili ni ombi langu kwako
Mungu akukumbuke na wewe
(Katembee nawe) Katembee na wewe
(Katembee nawe) Hata uwapo gizani akulinde
(Moyo wangu) Wewe u wimbo wangu
(Wewe ni bwana wangu) Tena dawa ya moyoni mwangu
(Wewe u fahari yangu) Ufahari yangu
Wewe u wimbo wangu
Wewe u thamani yangu
Wewe u mwaminifu wangu
Bwana wewe unaweza
Wewe ni Mungu uliye hai
Wewe ni mfalme wa ajabu
Wewe unayeponya mioyo
Wewe ni kisima kwako nitachota hekima
Kwako nitachota baraka
Kwako nitachota wema
Kwako nitachota ukuu
Kwakoo, kwako nitajifunza
Kwako nitaburudika
Aaaaaah!