![Taifa Letu](https://source.boomplaymusic.com/group10/M00/09/29/1f569376cb5b4308bad485f84bb6ce20.jpg)
Taifa Letu Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2021
Lyrics
Taifa Letu - Ambwene Mwasongwe
...
Iyeeeee Iyeeeee
Taifa letu, nyumbani kwetu
Tumepewa na Mungu
Fahari yetu, hazina yetu
Tumejengwa kindugu
Utu wetu, lugha yetu
Alama za tunu zetu
Ardhi yetu urithi wetu
Zilipofichwa mali
Akulinde mola
Akulinde
Akulinde
Akulinde mipaka yako
Akulinde mola
Akulinde anga lako
Akulinde
Akulinde mola
Tumeshaionja, Tanzania ya leo
Tumekula vya kwake
Tumekunywa vya kwake
Tanzania ya jana
Ilitengenezwa na wa jana
Tumeifaidi leo
Kwa kazi walioifanya
Tuwatengenezee wale wajao
Waikute iko salama
Tanzania ya neema
Tanzania yangu
Nakupenda, nakuombea
Akulinde mola
Akulinde
Alinde mipaka yako
Akulinde mola
Akulinde anga lako
Akulinde
Akulinde mola
*
Kinachoipa fahari nchi yetu
Sio pekee milima, mbuga na wanyama
Bali mioyo inayo ona fahari
Ya kuitwa mtanzania mzalendo
Kinachoipa ukubwa nchi yetu
Si mipaka pekee wala wingi wa watu
Ila ni moyo wa kukubali kufa kwa kupigania
maslahi yake
Akulinde mola
Akulinde
Tanzania yangu
Akulinde mola
Akulinde
Alinde Watoto wako wote
Akulinde mola
Mola akutunze
Akulinde
Iyeeiyeee
Akulinde mola
Akutendee mema
Akulinde
Akulinde nchi yangu
Uuhhoooohooo
Baba Mungu, Baba Mungu
... na machozi
Ya waliotuwekea misingi
Damu yao na machozi ikawe rutuba
Yakustawisha vizazi vijavyo
Ardhi yetu tuipandapo mbegu
(tuipandapo mbegu)
Ikatupe chakula cha kutosha
Ikawakatae wanaotaka vurugu ili
Nchi yetu idumu mileleee, Mola
Akulindee Mola-Akulinde Tanzania
Akulinde
Akulindee mola
Akulinde
Usipatwe na mabaya
(Akulindee mola)
Na magonjwa
Na ajali (Akulindee)
Na majanga
Yawe mbali nawe Tanzania
(Akulindee mola, Akulinde )
Tanzania yangu
Nakuombea kwa Mungu
(Iyee iyee iyee) akulinde
Mola, iyee iyee iyee iyee
Akulinde (iyee iyee iyee iyee)
Mipaka ya nchi yako
(iyeiyee)
Watu wako wote mola
A K U L I N D E!