![Mwana](https://source.boomplaymusic.com/group10/M00/07/21/4816bfd498944bcf91f6fe88a5c2c648.jpeg)
Mwana Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2020
Lyrics
Mwana - Joel Lwaga
...
nilifikiri moyoni mwangu
nikamwambia baba, nipe sehemu ya mali yangu,
nikaondoka nyumbani kwetu, nikaenda mbali
nikatumia mali yote
nikacheza na muda
nikaruhusu mali initawale
maisha yakawa magumu
nikafikiri moyoni mwangu
nitaenda wapi
nyumbani nimeshaondokaga
nitafanya nini mimi mwana mpotevu
nilipozingatia, moyoni mwangu mimi
nikaona bora nirudi kwa baba
yanini kuendelea Kula na nguruwe mahali hapa wakati watumishi wa baba nyumbani wanakula na kusaza
nikaona bora nirudi kwa baba
nitamwambia nimekosa juu ya mbingu na Mbele Yako, sistahili tena kuitwa mwanao
lakini baba aliponiona kutokea mbali akanikimbilia
akanivika mavazi mazuri na pete kidoleni mwangu
akanikumbatia na kunibusu shingoni akaamuru sherehe ifanyike maana mwanae aliyekufa sasa anaishi tena
mwanae aliyepotea amerudi
akasema sitakufanya kuwa mmoja wa wajakazi wangu
wewe ni mwanangu