
Wadumu milele Lyrics
- Genre:Afrobeats
- Year of Release:2017
Lyrics
Wadumu milele - Joel Lwaga
...
Msimamizi wa mipaka ya bahari
Utunzaye ghala ya mvua
Waamua vita ya jua na mwezi
Upepo na mawimbi vyakujua
Uketie mahali pa siri
Patakatifu palipoinuka
Wautangaza mwisho mwanzoni
Hakuna usilolijua
Nani wakulinganishwa Nawe
Jehovah mwenye nguvu?
Ufalme wako ni wa zamani zote
Vizazi vyoteeee
Miaka kwako sio umri
(miaka kwako sio umri)
Vizazi kwako si ukomo
(Vizazi kwako si ukomo) x2
Wadumu milele(wadumu milele) x4
Wewe Bwana ni kama maji
Maji yenye kina kitefu
Maji yenye kina kirefu
Kamwe hayapigi keleleee
Ni kweli kuna mabwana wengi
Lakini wewe ni Bwana wa mabwana
Ni kweli kuna miungu mingi
Lakini wewe ni Mungu wa miungu
Siku kwako sio vipindi
Majira kwako sio ishara
Hufikiwi kwa mnara wa Babeli
Jina lako ni ngome imaraaa
Nani wa kulinganishwa Nawe....
Miaka kwako sio umri....
Wadumu milele....
Wadumu milele...
Say Yeah( x8)
Nani wa kulinganishwa nawe
Jehovah mwenyenguvu
Ufalme wako ni wa milele yote
Bwanaaaa
(END)