Kazi Yako Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2013
Lyrics
Kazi Yako - Gloria Muliro
...
Kazi Yako by Gloria Muliro
{ Eeh Mungu eeh kazi yako haina makosa
Eeeh Mungu eeh utukuzwe kwa unayotenda } ×2
{ Mara nyingi mwanadamu, hayaelewi matendo yako
Anapopata matatizo, maswali tele moyoni,
Mbona yafanyike hivi, mbona yafanyike vile } ×2
Lakini baba mi najua kazi yako haina makosa
{ Eh Mungu eeh kazi yako haina makosa
Eeh Mungu eeh utukuzwe kwa unayotenda ) ×2
Maisha yangu mwanzoni, yalijawa kilio na dhiki
Nilisongwa songwa sana, na matatizo ya dunia hii
Nilipoteza tumaini, nikamuuliza Mungu maswali,
Mbona wainua wengine, mimi wanisahau?
Mbona wabariki wengine, mimi wanisahau?
Mbona wakumbuka wengine, mimi wanisahau?
Sikujua mi sikujua, alichokuwa akitenda Mungu
Leo hii natambua kazi yake haina makosa ( eeeh )
{ Eeh Mungu eeh kazi yako haina makosa
Eeeh Mungu eeh utukuzwe kwa unayotenda } ×2
{ Mwanadamu sinung'unike, wakati wewe humwelewi Mungu
Kwani yote hutendeka kwa wema, kwa wale wampendao Bwana,
Inua imani kwa Mungu, mtukuze kwa anayotenda} ×2 ( eeh )
{ Eeeh Mungu eeh kazi yako haina makosa
Eeeh Mungu eeh utukuzwe kwa unayotenda } ×2