![Unajikuta Wewe Nani](https://source.boomplaymusic.com/group10/M00/10/31/e9f3749e74b84f0ba5a0d971ec24e3de_464_464.jpg)
Unajikuta Wewe Nani Lyrics
- Genre:Afropop
- Year of Release:2022
Lyrics
Unajikuta Wewe Nani - Sabah Salum
...
Oooooh mmmmh
Mmmmh
Nimezipata salam sasa nakupa majibu
Siogopi mwanadamu nategemea wahabu
Nimezipata salamu sasa nakupa majibu
Siogopi mwanadamu nategemea wahabu
Nakula nakula nalala kwangu
Hunitishi hunitishie kwa lipi
Huijui huijui hatima yangu
Kivyovyote kivyovyote sikuogopi
Nashukuru napumua napata oxygen mola ananijaalia
Hauwezi kutibua aliyopanga manani ebu acha kujisumbua
...
Kiganjani huenei jeuri yatoka wapi
Punguza ugaigai nikuogope kwa lipi
Kiganjani huenei jeuri yatoka wapi
Ooh punguza ugaigai nikuogope kwa lipi
Nisile nisinywe maji kwa maneno yako tu
Uongo kwani kipaji na sio kwakila mtu
Ah hilo husilitaraji
Namuogopa mungu tu
Yeye ndie muumbaji
Nampaji wa kila kitu
Hilo husilitaraji
Namuogopa mungu tu
Yeye ndie muumbaji
Mpaji wa kila kitu
....
Unanipangu pakavu ulivyo haujijui
Husinipime ubavu milele haunisumbui
Unani pangu pakavu ulivyo haujijui
Husinipime ubavu milele haunisumbui
Ooh ilo unojivunia pumzi ya kwake mungu
Ata nami napumua niondolee kiwingu
Ilo unajivunia pumzi ya kwake mungu
Ata na mi napumua niondolee kiwingu
Wewe nani umekua wakuogopwa ni mungu
Yeye ndie anaetoa ridhiki yako na yangu
Wewe nani umekua wakuogopwa ni mungu
Yeye ndie anaetoa ridhiki yako na yangu
Mizigo ulojitwisha mingine si kazi yako
Hauna pumzisha nilipo na mungu yupo
Wapo wasokuogopa sio mm hasirani
Madaraka unajipa kwani umekua nani
............
Wameshindwa waloanza utaweza kitu gani
Kitambo nimekukuza haujai kiganjani
Aah nuna na ujivimbishe sikosi ridhiki yangu
Nani ata unitishe we kiumbe mwenzangu
Hao hao watingishe sijari nafanya yangu
Wameshindwa waloanza utaweza kitu gani
Kitambo nimekukuza haujai kiganjani
Ooh huwai kulizua aloandika manani
Linauma ninajua lakini ufanye nini
Sote tunategemea mwenzangu una nini
Wameshindwa waloanza utaweza kitu gani
Kitambo nimekukuza haujai kiganjani