Umuombe Mungu Lyrics
- Genre:Afrobeats
- Year of Release:2014
Lyrics
Umuombe Mungu - Upendo Nkone
...
lyric sync by Phellow Aduvaga 254790511905
Tatizo lako nini
mbona wewe unalalamika sana
umesema Mungu haoni mateso yako
umerudi nyuma kwa kisingizio kwamba Mungu hakujali
kumbe Mungu anakutazama
Neno lake lasema umwite siku ya mateso akuokoe
akuvushe ulipo uone nguvu zake
hata kama wamekunenea maneno mabaya ya laana
Mungu wetu anayaondoa
haijalishi unapita kwenye wakati gani
wewe omba (umuombe atakutendea)
magonjwa ya muda mrefu una maumivu sana wee omba
umuombe (omba) atakutendea
hauna pesa ni njaa kali unahangaika muombe Mungu
umuombe atakutendea
kila unalolofanya halifanikiwi kabisa usijali omba
umuombe atakutendea
umuombe Mungu wee
umuombe.....
Mungu anaweza
umuombe atakutendea
mwombe Mungu kwa unyenyekevu
umuombe (omba wee) umuombe Mungu anaweza yeyeyeyee
umuombe atakutendea
piga magoti mbele za Baba
umuombe.....
umuombe Mungu anaweza
umuombe atakutendea
anasikia, anajibu
umuombe....yeyeye...umuombe Mungu anaweza
umuombe atakutendea
****piano*****
*******verse2******
Ni jambo gani gumu
ambalo Mungu hawezi kulitenda
ni ugonjwa upi ambao hawezi kuuponya
umelia sana na tena umeteseka mno wewe
usijiue Mungu yupo
kwa kitambo kidogo amekuwacha
kwa rehema nyingi atakukusanya
kwa fadhili zake atakurehemu
Haijalishi unapita kwenye mapito gani
wee muombe Mungu wako
umuombe atakutendea
daktari amepima unao ugonjwa
akasema huwezi kupona mwachie Mungu
umuombe atakutendea
bosi wako kazini amesema kazini leo mwisho
Mungu ana njia....umuombe atakutendea
wamekunenea mabaya
wamesema huwezi kufanikiwa
mweleze Yesu wee...umuombe atakutendea
muombe Baba...umuombe...heiyeee
umuombe Mungu anaweza
umuombe atakutendea
omba..omba..omba...umuombe...omba...
umuombe Mungu anaweza...omba wee
umuombe atakutendea
mwombe Mungu kwa bidii...umuombe
funga na kuomba....umuombe Mungu anaweza
yeye anajibu....umuombe atakutendea
omba kama Hana...umuombe
omba kama Hezekia....umuombe Mungu anaweza
umuombe atakutendea
*********piano******
Hee! umuombe.....umuombe
umuombe Mungu anaweza. .heiyeee
umuombe atakutendea
kumbuka Suleimani aliomba hey!...umuombe
akapewa hekima....umuombe Mungu anaweza...yeyee
umuombe atakutendea...haiyaaa
Paulo na Sila ....umuombe ...waliomba gerezani....
umuombe Mungu anaweza...
....milango ya gereza ikafunguka...
umuombe atakutendea
na wewe omba...umuombe
Mungu ana jibu....umuombe Mungu anaweza
umuombe atakutendea.......
lyric sync by Phellow Aduvaga 254790511905
thanks for coming