Vilivyo Juu Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2021
Lyrics
Ulinitoa kwenye shimo la kifo
Ukanichukua kwa mkono
Na kunipa maisha
Mapenzi ya bure sikuyazoea
Ulikuwa mwangaza na taa
Kunionyesha njia
Neno lako linaniongoza
Kila siku majaribu ninayopitia
Uwepo wako umekuwa kwangu baraka
Nimejipata nina tamaa
Kukaa karibu nawe
Ninatazama mbele sirudi nyuma
Niko na wewe
Ninaangaza macho yangu
Kwa vitu vilivyo juu
Kwa Yesu ni tumaini
Ameketi enzini