Ombi Langu Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2021
Lyrics
Nionyeshe
Ajabu za Pendo lako
Niwe mboni ya jicho lako
Unifiche kwa mbawa zako
Yahweh
Niongoze
Mkono wako unitie nguvu
Neno lako liwe ngome yangu
Nikufuate ewe Mwanga wangu
Yahweh
Hili ombi langu
Wewe utukuzwe
Wewe wastahili
Yahweh
Yahweh
Nitakase
Umulike siri zangu za moyo
Unioshe kwa damu yako
Nitengeneze kwa moto wako
Nipendeze
Niinue
Univike kwa haki yako
Nionyeshe utukufu wako
Ukiketi kwenye enzi lako
Milele
Hili ombi langu
Wewe utukuzwe
Wewe wastahili
Yahweh
Yahweh