PENDO LA AJABU Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2024
Lyrics
Yesu pendo lako ni pendo la ajabu
Yesu pendo lako ni pendo la ajabu
Yesu pendo lako ni pendo la ajabu
Pendo ambalo sikupata ulimwenguni
Nilizunguka nikitafuta rafiki ooh
Nikazunguka nikitafuta mpenzi
Rafiki wote walikuwa ni waongo
Naye mpenzi kageuka kuwa hasidi
Waliniacha nikiwa hali mahututi
Niliodhani kuwa ni rafiki zangu
Naye mpenzi akaniharibia sifa
Yesu akaja kwa kweli 'kaniokoa
Yesu pendo lako ni pendo la ajabu
Yesu pendo lako ni pendo la ajabu
Yesu pendo lako ni pendo la ajabu
Pendo ambalo sikupata ulimwenguni
Na kitandani nilikuwa nimelazwa
Marafiki wakanitizama 'kaenda
Wakasema kweli huyu hawezipona
Lakini Yesu yeye hakuniacha
Korokoroni kwa kweli mi nilipofungwa
Hakuna aliyetaka kuhusishwa nami
Hakuna ndugu aliyenitembelea
Rafiki Yesu yeye hakuniacha
Yesu pendo lako ni pendo la ajabu
Yesu pendo lako ni pendo la ajabu
Yesu pendo lako ni pendo la ajabu
Pendo ambalo sikupata ulimwenguni
Na isitoshe baada ya haya yote
'Kanionyesha dhambi zangu huyu mpenzi
Akaniambia nikitubu 'taniokoa
Aniweke huru kisha anipe uhai
Niliyopata kwa Yesu ni ya ajabu
Upendo huu sijapata kuona mwingine
Sasa natangaza wote wakafahamu
Pendo la Yesu ni pendo la ajabu
Yesu pendo lako ni pendo la ajabu
Yesu pendo lako ni pendo la ajabu
Yesu pendo lako ni pendo la ajabu
Pendo ambalo sikupata ulimwenguni
Yesu pendo lako ni pendo la ajabu
Yesu pendo lako ni pendo la ajabu
Yesu pendo lako ni pendo la ajabu
Pendo ambalo sikupata ulimwenguni
Yesu pendo lako ni pendo la ajabu
Yesu pendo lako ni pendo la ajabu
Yesu pendo lako ni pendo la ajabu
Pendo ambalo sikupata ulimwenguni
Yesu pendo lako ni pendo la ajabu
Yesu pendo lako ni pendo la ajabu
Yesu pendo lako ni pendo la ajabu
Pendo ambalo sikupata ulimwenguni