RAFIKI (LIVE) Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2023
Lyrics
Dunia inisongapo hata ndugu zangu
Wanaponiacha katika taabu za dunia
Moyo wangu tulia roho yangu tulia
Unaye Kipenzi ni Yesu
Ninaye rafiki wa kweli
Rafiki anitulizaye moyo
Wale wanisemao na kunisimanga
Wajue Yesu ni rafiki
Yesu ni rafiki kweli Yeye haniachi
Baba hataniacha katika taabu za dunia
'Kiniona kwenye shida, huja karibu nami
Kwa kweli ninaye rafiki
Ninaye rafiki wa kweli
Rafiki anitulizaye moyo
Wale wanisemao na kunisimanga
Wajue Yesu ni rafiki
Namtangaza Yesu namuinua Yesu
Rafiki aliye nijia 'nishidani
Kanifunga vidonda 'kanonyesha mapenzi
Kwa kweli ninaye rafiki
Ninaye rafiki wa kweli
Rafiki anitulizaye moyo
Wale wanisemao na kunisimanga
Wajue Yesu ni rafiki