SINA CHA KUJIVUNIA Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2024
Lyrics
Sina cha kujivunia eeh mi sina cha kuringia
Yote mi niliyo nayo ni kwa neema ya Mungu
Baraka na ufanisi yale yote nilonayo
Sio kwa bidii yangu ni kwa neema ya Bwana
Hivyo ninamuinua Baba ninamshukuru
Natukuza jina lake Yeye pekee aishiye
Sina cha kujivunia mi sina cha kuringia
Yote mi ninayofanya ni kwa neema ya Mungu
Sina cha kujivunia mi sina cha kuringia
Yote mi ninayofanya ni kwa neema ya Mungu
Asante Baba wa milele kwa hiyo neema yako
Ulonipa ewe Baba nikatekeleze yote
Sio kwa ujuzi wangu wala si bidii yangu
Neema Yako juu yangu kweli ndio yanitosha
Hivyo nitakuimbia Baba nitakuinua
Kwa kweli nikushukuru kwani umenitendea
Sina cha kujivunia mi sina cha kuringia
Yote mi ninayofanya ni kwa neema ya Mungu
Sina cha kujivunia mi sina cha kuringia
Yote mi ninayofanya ni kwa neema ya Mungu
Tizama maisha yangu na yote nilopitia
Natambua sina nguvu neema Yako yanitosha
Hakuna nilivyo navyo ambavyo n'tajivunia
Kwani vyote hata nami sote Baba tu mali Yako
Hivyo nitakuimbia mimi nitakuinua
Baba nitakuishia Wewe ulonitendea
Sina cha kujivunia mi sina cha kuringia
Yote mi ninayofanya ni kwa neema ya Mungu
Sina cha kujivunia mi sina cha kuringia
Yote mi ninayofanya ni kwa neema ya Mungu
Sina Baba mimi sina uuhh vyote
Vyote ni vya Mungu wangu
Hata mimi pia eeh mimi mali yako
Vyote nilivyo navyo Baba
Vyote ni mali yako