Unayo Mapungufu Lyrics
- Genre:Taarab
- Year of Release:2023
Lyrics
Unayo Mapungufu - Jahazi Modern Taarab
...
........................................
Si kweli, unajinadi ujinga, huna huo, huna huo ukamilifu.
Si kamili sote tunaunga unga, tuna yetu, tuna yetu mapungufu.
Mkamili ni mmoja chinga chinga.
Mmoja tu Raufu Raufu.
Mkamili ni mmoja chinga chinga.
Mmoja tu Raufu Raufu.
Kilanilonalo unalo na wewe, tunapishana matumizi
Nililonalo ni langu mwenyewe, siri yake Mwenyezi
Kilanilonalo unalo na wewe, tunapishana matumizi
Nililonalo ni langu mwenyewe, siri yake Mwenyezi
Usinikomalie na mapungufu, ilhali ndio ubinaadamu
Usijishupalie ni mkamilifu, huna huo utimamu
Usinikomalie na mapungufu, ilhali ndio ubinaadamu
Usijishupalie ni mkamilifu, huna huo utimamu
Kuna kukosa na kupatia, huo sio upungufu, ni mazagazaga
Kukomaa na aliyeokosea, huo ndio udhaifu tena utamu kunoga.
Kuna kukosa na kupatia, huo sio upungufu, ni mazagazaga
Kukomaa na aliyeokosea, huo ndio udhaifu tena utamu kunoga.
Upungufu waja tumeumbiwa, mkamili Mola Raufu.
Si kweli hujatimia, una mengi mapungufu
Upungufu waja tumeumbiwa, mkamili Mola Raufu.
Si kweli hujatimia, una mengi mapungufu
Punguza kuzodoa, yangu mapungufu
Huna ulichotimia, acha majisifu
Punguza kuzodoa, yangu mapungufu
Huna ulichotimia, acha majisifu.
**Chorus.**
Una yako mapungufu, fahamu usitutoe
Mungu ndio mkamilifu, uzushi usituletee
Unayo
Yako mapungufu
Huna
Huo utukufu
Unayo
Yako mapungufu
Huna
Huo utukufu
........................................
Punguza sifa wewe, punguza nyodo wewe
Punguza sifa wewe, punguza nyodo wewe
Mafumbo unayofumba, si kwamimi
Madhali hujaniumba, funga ndimi
Punguza sifa wewe, punguza nyodo wewe
Punguza sifa wewe, punguza nyodo wewe
We punguza majisifu, we mangungu
Huna huo ukamilifu, we si Mungu
Punguza sifa wewe, punguza nyodo wewe
Punguza sifa wewe, punguza nyodo wewe