Kila saa Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2023
Lyrics
Jana imeshakuwa historia,
Kesho haijaahidiwa,
Ungali na nafasi, itika,
Yesu anapokuita njoo.
Kila saa anangoja ufanye uamuzi
Anasubiri akitamani urudi nyumbani.
Malaika, Jeshi la mbinguni,
Wameshika vinubi,
Wakisubiri kufanya shangwe pale unaporudi.
Bado hujachelewa kurudi miguuni pake.
Njoo hivyo ulivyo,
wewe ni wathamani.
Kila saa anangoja ufanye uamuzi
Anasubiri akitamani urudi nyumbani.
Malaika, Jeshi la mbinguni,
Wameshika vinubi,
Wakisubiri kufanya shangwe pale unaporudi.