Turudiane ft. Lava Lava Lyrics
- Genre:Bongo Flava
- Year of Release:2023
Lyrics
Turudiane ft. Lava Lava - D Voice
...
......
Lavalava:
nmekua bubu nmepigwa na butwaa
mdomo mzito kinywa kama ndondocha
macho yana magugu sioni mbele najikwaa
yani ujanja sina nmezorota
naona joto sijoto baridi sibaridi mwili wachoma choma
naona kichwa kinawaka moto moyo unakwenda speed yani homa sihoma
vipimo nmemaliza kwa manguli daktar waganga matabibu
kumbe najilimbikiza maumivu makali naongeza maswahbu
nmezunguka kote buza na yombo dovya sijaambulia chochote zaid ya kuchovychovy
rudi tuishi sote ujinga tu uliniponza jaribu kusahau yote mtima uje kupoza baby fanya..
turudiane, turudiane tena
turudiane..tuwe kama zaman
fanya turudiane turudiane tena(unirudie baby)
turudiane..tuwe kama zaman(turudiane)
.....
D voice:
yalopita yamepita sindwele rudi tugange yajayo we nmekuzoeaa
tufanye yamekwisha uje tujenge yambele yale tuachane nayo mwenzako najidodea.
rudi tufunike kombe mwanaharam apite tusijali tutaonekanaje kwa ndugu jamaa
nmekubali kwako kibonde acha tu nidhalilike
sina habari ata wakisemaje nachotaka furaha
yale matusi kejeli vijembe mafumbo kutupiana yote tufanye yaishe
najua twapendana kweli sasa ya nini tunazozana..rudi penzi tudumishe..
nmezunguka kote buza na yombo dovya sijaambulia chochote zaid ya kuchovychovy
rudi tuishi sote ujinga tu uliniponza jaribu kusahau yote mtima uje kupoza baby fanya..
turudiane, turudiane tena(turudiane tena)
turudiane..tuwe kama zaman
fanya turudiane turudiane tena(unirudie baby)
turudiane..tuwe kama zaman(turudianee)
.......