Nawaza Lyrics
- Genre:Bongo Flava
- Year of Release:2023
Lyrics
Nawaza - Barnaba
...
Yele yele yele wavejaa oooh waveja ooh
Yele yele yele wavejaa oooh waveja ooh
Tajiri rafiki yake pesa
Masikini rafiki yake uhai
Najiuliza yupi mwenye mana
Yule nilompenda jana ama waleo ama atakae kuja
Kuna muda najiuliza maswali
Wapi niliko sahihi wakati niliopo ama nilopita ama niendako
Nichagulieni majibu
Mwengine analilia kuolewa
Mwengine analiliaga taraka
Yupi yupo sahihi mwengine anachoma ubani
Yule anadate na jirani wakati ana mume ndani
Nakumbuka mama alinisihi mwanangu kua uyaone sio magorofa
Unaweza panda ngazi na kushuka
Maisha tambala bovu walio wengi wachovu so chunga sana
Sukari imepanda bei buku mbili
Mchana unapitaga sina dill
Ayaaa maisha gheto mabovu waliowengi wachovuu
Tunaunga unga mtaani
Life la mtaani gumu husitamani vingi vinapita
We ni mwanadamu kidogo chako lidhika
Ujui mwenzako wapi katoa eeh aaeeh
Dear God show me the good way
Dear God leave me the long way
Nataka fanya vingi in my life
Nataka niwe mwema in the eys
Binadamu walimkana yesu ww ni nani
Punguza kujifanya mwenye imani
Wakinuna na we nuna pia
Wakicheka nawe cheka pia
Mind your business hatulazimishani
Huwezi kua mwema kwa kila mtuu
Unanikosea alafu unataka nifanye utu
Roho mbaya haijengi ila inaepushaga mengiii
Maisha ya bongo yani popote kambi
Mtoto mdogo anambebda mwenye kitambi
Kwa heshima alitakiwa amwite baba huyo
Kwa phonebook amemsave baby huyo
Majabu ya musa hayaa
Neno urafiki na unafiki vimetofautiana herufi moja tu
Kua makini na unaosema unawaamini
Husijejutiaga mwenzangu na mimi
Somebody told me
Tafuta pesa Monday sio siku ya kazi
Na tukizipata tusifundishane kula bata
Hujanisaidia kutafuta
Soo punguza ushauri sasa
Sukari imepanda bei buku mbili
Mchana unapitaga sina dill
Ayaaa maisha gheto mabovu waliowengi wachovuu
Tunaunga unga mtaani
Dear God show me the good way
Dear God leave me the long way
Nataka fanya vingi in my life
Nataka niwe mwema in the eys