
Sitoamka ft. Lady Jaydee Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2002
Lyrics
Sitoamka ft. Lady Jaydee - MwanaFA
...
Chorus: Lady Jay Dee
Siku macho nikiyafumba,
Kama mimi sitoamka,
Taponiita Mfalme Muumba,
Japo shindwa mi kuinuka,
Verse I:
Toka uzazi wa Adamu,
Narithi yake damu maungo yangu yana timu,
Naiacha mbingu,
Nashuka duniani na naianza yangu zamu,
Nakua kama mdhaifu mwenye macho upofu,
Nilietoswa ndani ya mkondo wa maji ya kina kirefu,
Mionzi mikali toka angani kwa mtukuka,
Inawaka juu ya utosi ubongo wangu inamulika,
Napata ufunuo,
Upana wa upeo wangu unasitisha kawio,
Naanza nivuta nyayo toka giza la machweo,
Nakwea muelekeo, niikabili mitego na nione mwanga wa mawio,
Binadamu kwenye aridhi yenye rutuba,
Iliopambwa na vingi macho yangu ndo shuhuda,
Naishi naota ndoto natembea naitikia wito,
Nina malengo mazito na yenye tani si ya ratili uzito,
Nakua makini nisije zikosea kanuni nikawacha wanaonifuatia kwenye wingu la huzuni,
Napigania thabati nikae sawa na mstatiri,
Nizipokee salamu nikiwa ndani ya itishari,
Nihodhi makazi yangu kando ya ufukwe wa bahari,
Mikono yangu izungushe usukani wa motokari,
Mbolea ioteshayo fedha mifukoni niishamiri,
Mke mzuri, alie pambo nyumbani na watoto walionawiri,
Tupia macho takwimu,
Nakosa msukumo mimi mwana wa Adamu,
Kwani kasi inatisha, hatua nipigazo zi karibu kuhitimika,
Nabaki sikitika malengo hayatofika,
Maisha yangu yatakatika,
Roho itabaki natamalaki na mwili hautoamka.
Chorus: Lady Jay Dee
Siku macho nikiyafumba,
Kama mimi sitoamka,
Taponiita Mfalme Muumba,
Japo shindwa mi kuinuka,
Verse II:
Nautembeza mwili wangu mchovu,
Toka sulubu ya zahama zilizokwisha nisibu,
Fikira zabaki na yasofutika makovu, yenye ung'avu wa dira,
Ibainishayo kuwa ndani ya jasho langu ndimo ilimo thamani ya wangu ujira na akili na mali zangu ndo pekee vinara,
Katika hii ngumu imla,
Naufuta moyo jasho naujengea nguzo upate simama imara dhidi ya laghai za shetani,
Zinazonisakama na ziniandamazo,
Kwa ushawishi wa uzuri wa ndoto zinizongazo usingizini kunielekeza tamani,
Niifanye mikono yangu kwake Mungu alivyolaani,
Vyenye kutoka dhambini tavyonitoaa motoni,
Mimi muumini, tena mhanga mbele ya mola kwa shahada na sujudu ya sakafuni,
Narudisha kumbukumbu vitabuni,
Hap, Hapana Mola mwenye kuweza zaidi ya Manani,
Kwa mara nyingine mimi mja mtiifu narudi kwake,
Na hizi hatua chache zilizobakia kuyafikia makazi yake,
Naingia ndani ya msikiti,
Naketi juu ya busati, navuta uradi,
Kabla ya swala nautumai mkono wa mola mkombozi,
Ushike wangu utosi,
Anikirimu upesi,
Kwani kwake yote haya ni bado mepesi.
Chorus: Lady Jay Dee
Siku macho nikiyafumba,
Kama mimi sitoamka,
Taponiita Mfalme Muumba,
Japo shindwa mi kuinuka,