
Ungeniambia ft. Stara Thomas Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2003
Lyrics
Ungeniambia ft. Stara Thomas - MwanaFA
...
Chorus: Stara Thomas
Ungenipa kweli,
Kuwa kwako mi sina nafasi,
Kuliko kunipa mchanga wa macho na kuniacha,
Ungenambia, nambia.
Ungenipa kweli,
Kuwa kwako mi sina nafasi,
Kuliko kunipa mchanga wa macho na kuniacha,
Ungenambia, nambia.
Verse I:
Toka kwako siyaoni nilokua nayaona mwanzo,
Uliniacha nikaamini kuwa umeumbwa kwa ajili ya mimi,
Uliniacha nikasahau kuhusu mpenzi wangu wa zamani,
Sasa unafanya mapenzi kwangu yakose thamani,
Ungenambia, utakua nami ukinichoka utanitosa ukitosheka,
Pumbavu mimi,
Ningeiona kabla haijaja, nisingepoteza muda ningekuacha mara moja,
Upande huna msimamo na upande hujui ufanyacho,
Yaani upande akili hazimo na upande haujajua utakacho,
Hukumbuki ulipotoka na yote tuloyavuka,
Hukumbuki kwani wewe ulietamka kwangu umefika,
Ungenambia,
Mi ni mdoli ukiboreka ndo unanita,
Sasa nafahamu vizuri unapenda maisha ya fahari,
Ukisahau kuwa mali hazinunui mapenzi ya kweli,
Sawa mapenzi ni yako, nenda, maamuzi ni yako,
Na wale wanaohizi ni zako,
Ungenambia,
Kuwa unataka bwana lodi na sio mchoma makaa,
Na kwamba kwangu unazuga ikija dili unapotea,
Ila umenipa funzo na sasa najua,
I can turn a whore to a housewife,
Ungenambia huh.
Chorus: Stara Thomas
Ungenipa kweli,
Kuwa kwako mi sina nafasi,
Kuliko kunipa mchanga wa macho na kuniacha,
Ungenambia, nambia.
Ungenipa kweli,
Kuwa kwako mi sina nafasi,
Kuliko kunipa mchanga wa macho na kuniacha,
Ungenambia, nambia.
Verse II:
Sasa sitaki unipende, nataka unichukie,
Katafute kauli mbaya ndo uje unambie,
Sitakuonyesha machozi nafahamu hayatonisaidia,
Ila nakosa raha napongundua kilichoninyima penzi ni ufukara,
Unatumika tu kama kijiko cha hoteli,
Sawa, mzuri ila mchafu unipitie mbali,
Umenifunza kupenda kwa hadhari,
Unakosaje kukumbuka hifadhi ya pendo langu,
Au ndo umeota mabawa so hulitaki tena tundu,
Ungenambia,
Kwamba penzi lako hutoka kwa ofa ya bia au hata bure ukijisikia,
Ingekua yawezekana ningefuta yalotokea,
Mwili tulikua wote kifikra uliniacha pekee,
Nikuote hali unamuota mtu mwingine,
Nakuacha uende sikwepi kubaki mpweke,
Nnachotaka ni ukumbuke na moyo wako ukusute.
Chorus: Stara Thomas
Ungenipa kweli,
Kuwa kwako mi sina nafasi,
Kuliko kunipa mchanga wa macho na kuniacha,
Ungenambia, nambia.
Ungenipa kweli,
Kuwa kwako mi sina nafasi,
Kuliko kunipa mchanga wa macho na kuniacha,
Ungenambia, nambia.
Verse III:
Eti nikikuta mwenzangu nielewe so zamu yangu,
Ndo yanavyotakiwa kuwa? Au nini kwangu?
Najuta kusema I Love You, najuta kukufahamu,
Mwisho wa simulizi nzuri muhusika napata wazimu,
Ungenipa ukweli Mummy, ya kwamba mi ni kibonde,
Na huna mipango nami ila ulitaka mida iende,
Penzi la maisha yangu na dawa ya maumivu yangu,
Sikuamini kuwa ipo siku ntakuona sawa na changu,
Ulinifanya nikupende ulifanya nikakuamini,
Mara nyingi ulikua nami nikaacha uingie moyoni,
Kumbe nayaita maumivu naingiza penzi motoni,
(Ungenambia nambia)
Ukarimu wangu tafsiri ikawa udhaifu,
Naa kunyamaza kwangu ikaeleweka kuwa ni upofu,
Kama kitambaa cha giza usoni na kweli nilikua sioni,
Nashindwa kuelewa mpaka leo ilikua nini,
Simu ikilia amani imepotea,
Ingawa yangu ngejishauri kuipokea,
Bado nilivumilia,
Nikiamini kuwa ipo siku upande wangu utajutia,
Usingenipa moyo Mamaa, ungenambia huh!
Chorus: Stara Thomas
Ungenipa kweli,
Kuwa kwako mi sina nafasi,
Kuliko kunipa mchanga wa macho na kuniacha,
Ungenambia, nambia.
Ungenipa kweli,
Kuwa kwako mi sina nafasi,
Kuliko kunipa mchanga wa macho na kuniacha,
Ungenambia, nambia.