![Kaa Nao](https://source.boomplaymusic.com/group1/M00/42/56/rBEeMVl50RWAM7JgAAB3VUA4vUw069.jpg)
Kaa Nao Lyrics
- Genre:Afrobeats
- Year of Release:2017
Lyrics
Kaa Nao - Mwasiti
...
Ooo ooh.
Mmmmh...
Kama sio wewe,
nisingekuwa hapa.
Kuficha upele,
nisikune napowashwa. Kwahiyari yangu na mapenzi yangu.
Furaha ya mwewe, wapiganapo panzi porini.
Bora mwenyewe,
kuliko penzi lako asilani.
Kwenye mapenzi nilizaliwa,
isiwe sababu uninyanyase.
Kunipa sumu, ninywe maziwa.
Kwenye mapenzi bora nipotee.
(Uuuuh. uuu.)
Kama mapenzi ni adhabu,
moyo wako kaa nao.
Nimechoka Kungoja ngoja.
Moyo wako kaa nao...
Kama mapenzi ni adhabu,
moyo wako kaa nao.
Nimechoka Kuuguza donda.
Moyo wako kaa nao...
Kaa nao,
kaa nao kaa nao,
moyo kaa nao
Maumivu kuyashinda ni kazi,
Bora kuridhisha moyo.
Nisubiri thawabu labda utanisahau
ila ni kuulaghai moyo.
Walisema mengi,
kwake mi siwezi bila wewe.
Ukaniumiza mengi,
kwa imani sitoweza mwenyewe.
Nakubali kweli mapenzi maua,
Yanachanua na kunyauka.
Kwa pressure usijeniua, yakanifika,
roho ikan'toka.
Kwenye mapenzi nilizaliwa,
isiwe sababu uninyanyase.
Kunipa sumu, ninywe maziwa.
Kwenye mapenzi bora nipotee.
(Uuuuh. uuu.)
Kama mapenzi ni adhabu,
moyo wako kaa nao.
Nimechoka Kungoja ngoja.
Moyo wako kaa nao...
Kama mapenzi ni adhabu,
moyo wako kaa nao.
Nimechoka Kuuguza donda.
Moyo wako kaa nao...
Kaa nao, kaa nao kaa nao,
moyo kaa nao
Ouuuu... mmmmh...
Moyo wako kaa nao...
Nimechoka kungoja...
Moyo wako kaa nao...
Moiyoo, Moiyyyoo, kaa nao...
Moyo wako kaa nao...
Nimechoka kuuguza doondaa
. Moyo wako kaa nao.
Moiyoo, kaa naoo.