TUMECHAGULIWA Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2022
Lyrics
TUMECHAGULIWA - Paul Clement
...
Maamuzi ya Mungu hayategemei ushauri wa mwanadamu
Ingekuwa hivyo sisi wengine tusingechaguliwa
Wengi wangetupinga (mbele Yake)
Wangetusimanga (mbele Yake)
Wangetusema vibaya (mbele Yake)
Tusingechaguliwa
Ila Mungu haangalii cheo, elimu, pesa na vinavyoonekana kwa nje
Anatazama moyo
Mungu anapomchagua mtu hata kama ni mnyonge
(Humpa nguvu katika huo unyonge wake x2)
**CHORUS!!**
Tumechaguliwa na Mungu,
Hatukuchaguliwa na wanadamu ..
Haijalishi tu' wanyonge ila tumechaguliwa
Mungu hatazami kama mwanadamu,
Anatazama kwa jicho la haki,
Asichopenda mwanadamu, Mungu ndicho anachopenda
Mungu alimchagua Musa mwenye kigugumizi cha kusema
Aongoze taifa kubwa kwa jinsi alivyo
Mungu alimchagua Daudi
ambaye hata hakuhesabika katika hesabu ya watoto wa nyumba ya Yesse baba yake
Sababu Mungu haangalii cheo, elimu, pesa na vinavyoonekana kwa nje anatazama moyo..
Mungu anapomchagua mtu hata kama ni mnyonge
(Humpa nguvu katika huo unyonge wake x2)
** Back to Chorus **
Tumechaguliwa na Mungu,
Hatukuchaguliwa na wanadamu ..
Haijalishi tu' wanyonge ila tumechaguliwa x4