Au ft. Nurwell Lyrics
- Genre:World Music/Folklore
- Year of Release:2022
Lyrics
Au ft. Nurwell - Nikki Mbishi
...
Yeah.. aah (ooooh)
I’m curious I wanna know (oooh mama)
Au labda hunipendi, ndo sababu unanitema
Hupendi ninavyoatend, alfajiri na mapema
Unaniacha stendi, njia panda niko dilema
Kutwa spendi weekend, kwako haijakaa njema
Au kisa silipuki, daily mitumba midosho
Ukiniona huzuzuki, sana sana unaona michosho
Bling bling sinyuki, sina mvuto sitoki smart
Mrefu sio mfupi, bora ningekuwa saizi ya kati
Au sikuvutii, ndio maana hunipi uthamani
Kioja ndani ya jamii, na kwanza haturandani
Pia hujisikii, kuwa na kapuku kama mimi
Ambae mswaki situmii, sina hadhi ya kunyonya ulimi
Au mpaka mavumba, ndo mapenzi yashamiri
Hata suala la unyumba, mpaka kwa muda ufikiri
Au umepata mchumba, mjanja tena tajiri
Sio mimi katumba, mla ganja nisie na dili
Au sijui mahaba, kitandani sikuridhishi
Sikuombi nakaba, tendo la ndoa kwa ubishi
Siwezi kubembeleza, kiupole ama siimbishi
Au sijui kuchombeza, kileleni sikufikishi
Au mama kukufuata ninakuchosha
Au tena we unaomba usinione tena
Au mama kukufuata ninakuchosha
Au tena we unaomba usinione tena
Au sababu mi wa bara, mwenzangu unatoka pwani
Ndo maana unaniona fala, wakati wa mambo flani
Niambie, ka siko imara kasoro weka hadharani
Nipunguze papara, nichezapo mechi uwanjani
Au umechoka ukonga, tukaishi kimara
Milima ya kitonga au safu za usagara
Hutaki niendeshe honda, unataka nidrive vitara
Haupendi samaki ng’onda, nikupe sato sangara
Au niache muziki, tushinde tu chumbani
Ufurahi kumuona nikki hakiwa hatoki ndani
Tukiandamwa na dhiki tutaishi maisha gani
Kiundani haifikiriki ya mbele mbona hutazami
Au sio nyota yangu, nimepiga wrong number
Nakuforce uwe wangu, damu zetu haziendi sambamba
Nimekuja na mkuki nataka kuutoboa mwamba
Wakati wenye bunduki mbele yako wameshindwa tamba
Wivu umezidi upendo ni uvivu zaidi ya vitendo
Kila siku lawama na kunizushia skendo
Kama hunitaki ni vema uniweke wazi
Nijue nitambue kwani mademu wapo shazi
Kwani vipi unayofanya mbona mchizi sikuelewi
Haki yangu hunipi hata mahitaji yangu ya msingi sipewi
Kwani vipi unayofanya mbona mchizi sikuelewi
Haki yangu hunipi hata mahitaji yangu ya msingi sipewi
Au mama kukufuata ninakuchosha
Au tena we unaomba usinione tena
Au mama kukufuata ninakuchosha
Au tena we unaomba usinione tena
Au kisa msanii unahisi wenzako watakupiku
Mchizi huniaminii, show za mkoa ama za usiku
Nitakupa HIV sababu mchapa nje ya ndoa
Changu sidime milupo vicheche makabakoa
Au labda situngi, mashairi ya kukusifu
Sina sony sifungi, hisia zangu kwako hafifu
Natafuna mirungi, uswahilini ni mtu wa tifu
Lakini sijidungi, huo ndo ukweli yakinifu
Au labda umenichoka, ila hutaki kunieleza
Kwamba nikki ondoka, me nimeshapata mwenza
Mbona mchizi nang’oka, kisha michongo nasebenza
Kwani mapenzi ya nyoka, si kwenye majani kuteleza
Hivi ni hiyari yako, au ulinipenda kwa shinikizo
Kutoka kwa rafiki zako, uliokuwa nao enzi hizo
Si ulifuata medako na wekundu wa mfululizo
Utizime hazma yako, pesa zangu zimekwenda likizo
Fikra ndani ya medula tamati picha samati
Wa chuya umeula eeh si hunipendi kwa dhati
Binadamu kwa sura, kiundani una roho ya nyati
Unanichezea sangula, hujui unanipotezea wakati
Au mama kukufuata ninakuchosha
Au tena we unaomba usinione tena
Au mama kukufuata ninakuchosha
Au tena we unaomba usinione tena
Au mama kukufuata ninakuchosha
Au tena we unaomba usinione tena
Au mama kukufuata ninakuchosha
Au tena we unaomba usinione tena
By Mugizi Jr.