Kijusi ft. Dannie Sepetu Lyrics
- Genre:World Music/Folklore
- Year of Release:2022
Lyrics
Kijusi ft. Dannie Sepetu - Nikki Mbishi
...
yeah,
kijusi.
yeah, aah aah
Mara ya kwanza mmekutana kwenye ukumbi wa starehe
nilikuwa mdogo sana, sikumbuki hata tarehe
mama alikuwa msichana mbichi aliyevunja ungo
enzi hizo baba kijana, *** mwendo mdundo
kila siku misele kwenu wanakula mingo
ukipishana nae lazima atageuza shingo
kweli ulimtia husuda na kumfanya adate
alipoteza fedha na muda ili akupate
sio picha la kivita, Bali bonge la drama
siku zikapita maskani baba ukahama
chumba ulipanga na kwao ilikua karibu
ukajenga mazoea na utani wa taratibu
ukaanza kwenda race, kushinda waruka vihunzi
wala hukujali kesi ya kutoka na mwanafunzi
Mara umletee zawadi na vitu vya thamani
zaidi ya maua na kadi ili kwako ajenge imani
mama alikuwa mtashi na mwepesi wa kuelewa
mashaka na wasiwasi moyoni vikaondolewa
ukamuona almasi na kwako zaidi ya ngekewa
na mwisho ukampa nafasi, na mapenzi ukanogewa
mapenzi yaligeuka ukimwi nikatengwa mfano wa virusi
nikingamu kijisusi, mtazamo kwa kamusi
mashtaka bila hatia, yanapaswa kutuhumiwa
mimi ndiyo kijusi.
niliyenyimwa haki ya kuzaliwa
haki ya kuzaliwa.
yeah!