Maji Ni Uhai Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2021
Lyrics
Maji Ni Uhai - Nikki Mbishi
...
Uh!
Unju
Wa miujiza kwenye beat,
Uh.. Hisia za Nyerere Butiama,
Upo Single? Tafuta ambaye mnavutiana
Mapenzi ni kutiana Moyo,
Bata kuspend kuchukiana , These hoes ain't loyal,
Punguza jazba, Bwaga Moyo
Wachumba wapo nasty kwa stage wanamwaga nyoro, Industry imejaa wachoyo, machawa na makolo, Mbwiga
Acheni Ngada vuteni wida,
Message sent, juu ya mdundo wa Uno so Mesen check,
Unju nukta mwisho wa sentensi, Aha na hii ndio maana, Raisi Obama halafu gaidi Osama,
Kwenda feki wanasema kukaba soko, Msanii ana stress Meneja uko Bar na Totoz,
Nawapa chapaa za moto, Kesi PCCB ya China CCTV vina sivisikii,
Uh.. Ukiulizwa nafanya hit song, Naleta Kosovo Ndanda Chitoto ping pong, Mpaka Korea Kaskazini kwa Kim Jong, Naumia kujua Chidi vits ndio yule King Kong
Maji ni uhai lakini ukizama baharini unakufa, (× 4)
Niko backstage mi na warm up, Sober na soda na donut na kwa kona,
Promota na performer reporter nakusoma,
Wote wapo high wanamoka na kunyonya,
Okoka na kuponywa ropoka nakuona,
Urekebishaji toboka nakushona,
Maradona soka mara kala kona chopa,
Alianza akiwa choka ghafla mara mona lofa,
Mic na beat ni mkate na divai, Karibu kwenye karamu vichache havifai,
Vichache havifai labda viwe vya msingi kama jiwe kwa mzinzi au heshima kwa ushindi,
Ukinicopy nakuzima ka muhindi mi ni boss kwenye rap, na hunikosi kwenye map,
Unapoteza muda kwa kuchat na ma ghost wa Snapchat, Haujifunzi kitu Man you're f***d up
Maji ni uhai lakini ukizama baharini unakufa (x 4)
Naishi na makarao Nikki Mbishi madharau, Baada ya Jeez Mabovu nadiss nasahau, Uliza Nay wewe!
Unju ni lakuchumpa usiingie kwa pupa uliza bei wewe, Gay wewe!
Umesahau jinsia kitaani unaitwa Omari huku unajiita Cynthia,
Nasinzia nikikuwaza, Nameless
Sister Duu simu nakukatia nikikukaza you're brainless,
Hata sijui naitwa nani, Unju natokea taifa gani, Bongo
Ni lazima kutumika wazee wa nusu nusu wamebaki nusu lita, Na kuhusu kunusurika hilo suala wasahau, Hivi we ni dogo Hamidu au Lil Bow Wow?
Unju bahau kale, Mwenyezi mungu siku ya kiama nakuomba usimsahau Babu Tale,
Maji ni uhai lakini ukizama baharini unakufa (x 4)