![Nisaidie](https://source.boomplaymusic.com/group1/M00/11/86/rBEeMljvTrKAQ25wAACsznxWmH0565.jpg)
Nisaidie Lyrics
- Genre:Pop
- Year of Release:2017
Lyrics
Nisaidie - Pitson
...
Nisaidie Baba, nisiwahi lala njaa
Nisaidie Baba, nisipatwe na balaa
Hasara iwe mbali na me, hata kwa biashara
Ninachouza wanunue; nisibaki na bidhaa
Nisiwahi kosa pesa za kulipa nyumba ya kukodisha
Pia unipe yangu, nisiishi sana ya kukodisha
Jinsi ya kupata dough; wewe Baba ndiyo, utanionyesha
Utatoa vitu vinavyo-nikondesha
Aa, aa, aa, aa, aa (Nisaidie)
Aa, aa, aa, aa, aa, aa (Nisaidie)
Aa, aa, aa, aa, aa (Nisaidie)
Aa, aa, aa, aa, aa, aa, aa (Nisaidie)
Itakuwaje baba? Jirani wanajua nimeokoka,
Na vile mimi ninateseka: niko na deni hata kwa mama mboga
Wameshanidharau, watakudharau
Mungu wa Ibrahimu, waonyeshe kwamba hujanisahau
Kama Shadrack, Meshack, Abedinego, hata wanirushe kwenye moto
Nikikosa ya dunia, bado sitawainamia
Aa, aa, aa, aa, aa (Nisaidie)
Aa, aa, aa, aa, aa, aa (Nisaidie)
Aa, aa, aa, aa, aa (Nisaidie)
Aa, aa, aa, aa, aa, aa, aa (Nisaidie)
Shadrack, Meshack, Abedinego, hata wanirushe kwenye moto
Nikikosa ya dunia, bado sitawainamia
Kwa kila kitu nifanyacho, Baba, nisaidie (nisaidie)
Kwa kila kitu nifanyacho, Baba, nisaidie (nisaidie)
Kwa kazi ya mikono yangu, Baba, nisaidie (nisaidie)
Kwa kila kitu nifanyacho, Baba, nisaidie (nisaidie)
Uniweke mbali na balaa, unisaidie (nisaidie)
Niweke mbali na hasara, Baba, nisaidie (nisaidie)
Kwa kila kitu nifanyacho, Baba, nisaidie (nisaidie)
Nisaidie, nisaidie, nisaidie (nisaidie)