
Wastahili Ibada Yetu Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2025
Lyrics
Ewe Bwana
Mungu wetu
Ni wewe tu watawala
Umeketi kwenye kiti cha enzi
Hakuna mwenye kukushinda
Umetukuka, Umejaa utukufu
Hakuna aliye kama wewe
Mungu wa ajabu
Umetukuka, Umejaa utukufu
Mwaminifu, Mwaminifu
Ni wewe pekee usiyekoma kutenda mema
Unastahili heshima na sifa zote
Milele tutaimba utukufu wako
Tunaungana na malaika
Na wazee ishirini na wanne
Na viumbe wanne
Tukiinuka na kuinama tukisema
Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu
Ni Wewe uketiye kwenye kiti cha enzi
Mwaminifu, Mwaminifu
Ni wewe pekee usiyekoma kutenda mema
Unastahili heshima na sifa zote
Milele tutaimba utukufu wako
Kwa sauti moja tunakuabudu
Kwa mioyo safi tunainua jina lako
Ni wewe pekee unastahili sifa na heshima
Milele na milele, Amina
Mwaminifu, Mwaminifu
Ni wewe pekee usiyekoma kutenda mema
Unastahili heshima na sifa zote
Milele tutaimba utukufu wako
Ee Bwana
Mungu wetu, tunakushukuru
Kwa wema na neema zako zisizokoma
Tunaomba utubariki na tuweze kukusifu
Milele na milele, Amina
Ee Bwana
Mungu wetu, tunakushukuru
Kwa wema na neema zako zisizokoma
Tunaomba utubariki na tuweze kukusifu
Milele na milele, Amina