
Twakuabudu Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2024
Lyrics
Twainama tukiinuka (tukiinuka kwako Yesu)
Twakutukuza (Ewe Mungu mwenye mamlaka)
Hakuna Hakuna (Hakuna aliye kama wewe)
Amina (Halleluya milele twakuabudu)
Tutaimba sifa zako
Tutakuabudu ewe Mungu
Mtawala wa vyovyote
Hakuna kama wewe
Mungu, sifa zako
Tutakuabudu ewe Mungu
Mtawala wa vyovyote
Hakuna kama wewe
Mbingu zakusifu (kwa utukufu wako zang'aa)
Viumbe na wazee wanne (wote wakuabudu we Mungu)
Hakuna (anayetamalaki wa kuabudiwa)
Twakusifu, twainama twakusifu, twainama tukisujudu, wewe tu wastahili)
Sisi wana wako (tutakusifu Bwana Milele)
Kwani wewe (ndiwe wa kupewa sifa zote)
Hakuna (Hakuna mwingine anayestahili)
Kuabudiwa (ila wewe Mungu wa miungu)
Amina tunakusifu
Twakupa zote sifa
Ibada yetu yote ni kwako
Ewe Mungu wa milele
Tutaimba sifa zako
Tutakuabudu ewe Mungu
Mtawala wa vyote
Hakuna kama wewe
Tutakuabudu (nani mwingine ila wewe)
Tutakusifu (Tutakupa sifa zetu zote)
Twakusujudu,
Pokea ibada, Pokea sifa, twakupa ewe Bwana, Mungu wa milele, (Wastahili)
Sisi wana wako (tutakusifu Bwana Milele)
Kwani wewe (ndiwe wa kupewa sifa zote)
Hakuna (Hakuna mwingine anayestahili)
Kuabudiwa (ila wewe Mungu)
Tutaimba sifa zako
Tutakuabudu ewe Mungu
Mtawala wa vyote
Hakuna kama wewe
Tutaimba sifa zako
Tutakuabudu ewe Mungu
Mtawala wa vyote
Hakuna kama wewe