
Neema Yako Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2025
Lyrics
Ewe Bwana, Mkombozi wangu
Yesu Kristu, nakuabudu
Wewe ndiwe mfalme wa mfalme
Nafurahi kuwa wako
Damu Yako imeniosha
Nimekuwa mpya kabisa
Neema Yako inanifanya
Kuwa mtoto wa Mungu
Uliponya majeraha yangu
Ukanitoa katika giza
Umenipa uhai mpya
Na furaha isiyoisha
Katika utukufu wako
Nitakuimbia milele
Wewe ndiwe Mungu wa miujiza
Mkombozi wangu wa kweli
Ewe Bwana, Mkombozi wangu
Yesu Kristu, nakuabudu
Wewe ndiwe Mfalme wa MFALME
Nafurahi kuwa wako
Hallelujah