
NAKUHITAJI Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2024
Lyrics
Nakuhitaji moyoni mwangu eeh Baba
Wewe pekee unipendaye kwa dhati
Nakuhitaji moyoni mwangu eeh Baba
Wewe pekee unipendaye kwa dhati
Wazazi wangu lazima wangenipenda
Kwa sababu mimi ni mwana wao
Ndugu zangu hawangekosa kunipenda
Walijipata tumezaliwa pamoja
Marafiki nao wakanipenda
Kila mtu sababu yake mwenyewe
Lakini Yesu upendo wako wa ajabu
Unanipenda upendo wa agape eeh
Nakuhitaji moyoni mwangu eeh Baba
Wewe pekee unipendaye kwa dhati
Nakuhitaji moyoni mwangu eeh Baba
Wewe pekee unipendaye kwa dhati
Ni Yesu pekee anipendaye Mungu wangu
Naye hajali katika hali niliyomo
Niwe mgonjwa Yesu Baba bado rafiki
Niwe na afya bado Baba ananipenda
Niwe na mali Yesu huwa karibu nami
Nifilisike bado Baba ananipenda
Yeye Baba upendo wake upo nami
Ananipenda upendo wa agape eeh
Nakuhitaji moyoni mwangu eeh Baba
Wewe pekee unipendaye kwa dhati
Nakuhitaji moyoni mwangu eeh Baba
Wewe pekee unipendaye kwa dhati
Kunao wengi watakupenda ndugu yangu
Mradi wewe una pesa una mali
Kunao wengi watakupenda dada yangu
Mradi wewe afya yako haina shida
Lakini siku 'taangukia katika shida
Marafiki wote watakutoroka
Huyu Yesu upendo wake ni daima
Anakupenda upendo wa agape eeh
Nakuhitaji moyoni mwangu eeh Baba
Wewe pekee unipendaye kwa dhati
Nakuhitaji moyoni mwangu eeh Baba
Wewe pekee unipendaye kwa dhati
Nakuhitaji moyoni mwangu eeh Baba
Wewe pekee unipendaye kwa dhati
Nakuhitaji moyoni mwangu eeh Baba
Wewe pekee unipendaye kwa dhati
Nakuhitaji moyoni mwangu eeh Baba
Wewe pekee unipendaye kwa dhati
Nakuhitaji moyoni mwangu eeh Baba
Wewe pekee unipendaye kwa dhati
Eeehh Wanipenda
Wanipenda Yesu
Wanipenda Baba
Nakuhitaji
Ingia moyoni mwangu
Eeeh Baba tenda yale utakayo
Wanipenda kwa dhati