NUSURU MOYO Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2024
Lyrics
Maisha yangu mi na Yesu sijuti wala sitojuta
Japo shetani hun'andama Yesu wangu yee hunilinda
Ulingo wa damu Yake huniepusha na madhara
Kati ya moto mi hupita natoka nikiwa salama
Maana hii damu ya Yesu ina uwezo wa kulinda
Kunusuru pia kuponya ndio ilo ninusuru
Kunusuru pia kuponya ndio ilo ninusuru
Nakwambia ndio ilo ninusuru
Mbali na Wewe nisimame mimi nitaangamia
Karibu Nawe nisogee niunusuru moyo wangu
Mbali na Wewe nisimame mimi nitaangamia
Karibu Nawe nisogee niunusuru moyo wangu
Kijana usidanganyike huko uendako ni kubaya
Unawaita marafiki na huku wanakupotosha
Pombe madawa ya kulevya na uzinzi utakwangamiza
Sogea karibu na Yesu utoswe ndani ya damu Yake
Hapo utapata amani na uhakika wa kuishi
Na utaimba wimbo mpya amenusuru maisha yako
Na utaimba wimbo mpya amenusuru maisha yako
Eeh mwanangu amenusuru maisha yako
Mbali na Wewe nisimame mimi nitaangamia
Karibu Nawe nisogee niunusuru moyo wangu
Mbali na Wewe nisimame mimi nitaangamia
Karibu Nawe nisogee niunusuru moyo wangu
Mbali na Wewe nisimame mimi nitaangamia
Karibu Nawe nisogee niunusuru moyo wangu
Mbali na Wewe nisimame mimi nitaangamia
Karibu Nawe nisogee niunusuru moyo wangu
Ukiniona nimesimama mbali na Yesu
Usicheke nasogea
Yesu wangu aninusuru an'okoe
Hunilinda na damu Yake Baba
Ameniokoa Baba
Yesu wangu
Mbali na Wewe nisimame mimi nitaangamia
Karibu Nawe nisogee niunusuru moyo wangu
Mbali na Wewe nisimame mimi nitaangamia
Karibu Nawe nisogee niunusuru moyo wangu
Niunusuru moyo wangu (Miguuni pako nasogea ewee Yesu wangu)
Niunusuru moyo wangu (Karibu na Wewe nitaishi mimi Baba yangu)
Niunusuru moyo wangu (Msalabani pako nitazitua hizi dhambi zangu eeh)
Niunusuru moyo wangu (Aaaiii Baba nitasogea)