Simba Vs Yanga (feat. Sixtonny) Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2023
Lyrics
Simba Vs Yanga (feat. Sixtonny) - Many Jay
...
(Many Jay)::Ah Simba Ball ni Pass pass pass,
sio kama Utopolo mnabutuabutua;
Tunawinda Ball bila Wasiwasi waaas
hata mkaze minyororo sisi tunaifungua:
Nyie ndio Wapinzani Gani? “ETI”
maana hata hamjulikani “ETI”
Simba huko Duniani,tunajulikana
nyie hamuonekani:
(Sixtonny)::Umesema tunabutuabutua ?”Sawaa”
ila Ubingwa twachukuwa “sawa”
na kuhusu kujulikana hizo ndoto za mchana
Dunia inatujuwa
Oya nyie makolo mmeshuka Chart
ona sasa mnajivunia Pass
kwani nini faida ya Pass ?
kazi yake kubwa si ni Kunyoshea Mashati ?
Chorus (sixtonny):: oyaa eeh Huku Jangwani Kutamu “aaah Jangwani kutamu”
Kushabikia Yanga ni Utamu “utamUtamutam”
(Many Jay) Oya eeh Huku maimbazi kutamu
“aaah Msimbazi kutamu”
kushabikia Simba ni utamu “utamutamutam”
Verse 2:(sixtonny)
Kwanza rangi yetu Black,njano na kijani
ipo mpaka kwenye bendera ya nchi,
Yanga tunapendwa sana Bala visiwani,
ndiomaana tukaitwa Wananchi.
Rangi nyeupe inapendwa na waganga,
Rangi nyekundu inaashilia majanga:
nyie makolo mnapendwa na washamba,
ndiomaana Diamond akaamua Kuja Yanga:
(Many Jay)Rangi nyekundu inawakilisha upendo bro
Rangi nyeupe ipo kwenye kanzu na majoho
alafu washamba ndio wanapenda utopolo
ndiomaana kati yenu wote hakuna mjanja kama mo.
Utopolo kazi yenu kulopoka,mkiishiwa point
ni Pumba zinawatoka,
ona mnaringia Rangi sio soka
kijani na manjano si Rangi ya Nyokanyoka ?
Chorus (sixtonny):: oyaa eeh Huku Jangwani Kutamu “aaah Jangwani kutamu”
Kushabikia Yanga ni Utamu “utamUtamutam”
(Many Jay) Oya eeh Huku maimbazi kutamu
“aaah Msimbazi kutamu”
kushabikia Simba ni utamu “utamutamutam”