Bwana Nakuhitaji Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2023
Lyrics
Jambo gani litakalo kuzuia kuzishika kanuni zake Bwana,
Je ni ulevi uasherati, uzinzi tamaa ya mwili au kiburi,
Hizo zote ni hila zake mwovu, awavuruge na kuwatawanya wakristo,
Simama wima kwenye imani,Umtazame kristo jemedari
Kila saa bwana wangu mimi ninakuhitaji,
Mi' mpofu masikini unishike mkono,
Kwako napata nguvu,waniinua nikianguka,
Nivute kwa kamba zako unisogeze kwako.
Mbele yangu kukiwa na giza nene,
Sehemu yangu nayo iwe ngumu,
Yakija machungu ya kunivunja moyo,
Macho yangu ninakuelekezea,
Wewe bwana unapo yaongoza,
Mapito yangu hakika ninakwenda salama,
Nenda nami nilinde siku zote nuru yako ikaniangazie.
Kila saa bwana wangu mimi ninakuhitaji,
Mi' mpofu masikini unishike mkono,
Kwako napata nguvu,waniinua nikianguka,
Nivute kwa kamba zako unisogeze kwako.