DAIMA Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2023
Lyrics
Eeh Jehovah Jireh Mungu wangu
Uketiye kitini cha enzi
Mbele zako mi ninasujudu
Wee ulo Mfalme wa wafalme
Eeh Baba yangu unapendeza
Eeh Mungu wangu waheshimika
Uweponi wako nasimama
Moyo wangu upate furaha
Daima nitakuinua
Daima nitakuinamia
Daima mi nitakusujudu eeh
Daima mi nitakuimbia
Wee Muumba vyote mweza yote
Unenayo yote hutimia
Neno lako sawa nawe Baba
Hata wafalme walitambua
Maji baharini yasikia
Amri yako wee unaponena
Hata na dhoruba hutulia
Isikiapo sauti yako
Daima nitakuinua
Daima nitakuinamia
Daima mi nitakusujudu eeh
Daima mi nitakuimbia
Umetukuzwa wee toka jadi
Mbingu na dunia zafahamu
Masherafi nao makerubi
Waimba sifa'zo juu mbinguni
Duniani ndege wakusifu
Samaki majini wasujudu
Milima imesimama wima
Yangoja ukague gwaride
Duniani nasi twakusifu
Wee ulo Mfalme wa wafalme
Wanadamu sote twakusifu
Kwa sauti na matendo yetu
Daima nitakuinua
Daima nitakuinamia
Daima mi nitakusujudu eeh
Daima mi nitakuimbia
Daima nitakuinua
Daima nitakuinamia
Daima mi nitakusujudu eeh
Daima mi nitakuimbia
Daima dawama nakuimbia Baba
Mi nitakuimbia
Mwamba wangu nakushujudu uishie
Mi nitakuimbia
Sauti yangu maishani mwangu nikuimbie
Mi nitakuimbia
Nikuabudu nikuinue Mungu wangu
Mi nitakuimbia