![Nikilala](https://source.boomplaymusic.com/group10/M00/03/09/6ac614becbcd43238949ed858a72a9a1_464_464.jpg)
Nikilala Lyrics
- Genre:Bongo Flava
- Year of Release:2023
Lyrics
Nikilala - Mocco Genius
...
Mmh silali ata nkizima taa
Kitandani namuona amekaa
Amenuna amechachamaa
Eti kwanini nimkoseshe raha
Kama we bado unakinyongo jua huku kinanisurubu
Kweli nisiwe muongo nateseka natamani nitubu
Nikilala naota naota unanimwagia tindikali
Nashtuka naogopa jasho lanitiririka silali
Mana nikilala tu tu tu, nikilala tu tutu
Nikilala tu
Naota unanikimbiza
Nikilala tu
Unataka kunichinja
Mana nikilala tu tu tu, nikilala tu tu tu
Nikilala tu
Unalia unaniuliza
Nikilala tu
Why nilikuumiza
Kama tatizo tendo wote utamu tuliupataga
Ama tatizo muda wako ata wangu uliutumiaga
Au nilivyokuacha hukuridhia moyoni ulikunja ulinkunjia
Imekua tabu ata nkisinzia naona sura yako inanijia
Ama tuseme mwenyezi amepanga kunikomesha
Ili nikipata mwengine nisidiriki kumtesa
Nikilala naota naota unanimwagia tindikali
Nashtuka naogopa jasho lanitiririka silali
Mana nikilala tu tu tu, nikilala tu tutu
Nikilala tu
Naota unanikimbiza
Nikilala tu
Unataka kunichinja
Mana nikilala tu tu tu, nikilala tu tu tu
Nikilala tu
Unanita unaniuliza
Nikilala tu
Why nilikuumiza