ONYESHA UWEZO Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2024
Lyrics
ONESHA UWEZO
Ota ndevu me naota ndoto za kuwa hero,
Ukienda vitani ukitegemea kupata droo,
Hizo ni hadithi za bunwasi zisizo na kikomo,
Ukinichukulia pouwa bac nichukulie na mambo,
Japo nishakula sana sitori lakn sina kitambi,
Wala sinenepi zaidi ya six packs nilizo nazo hizi,
Ukiniambia kwamba hadi narudi home usiku sometime siheshimu,
Nakwambia kuwa acha umbea kwenye jambo usilofahamu,
Maana jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza totoro,
Usiwe teja wakati huna undugu na wateja,bro
Muda haisimamii hata ufulie nguo saa,
Sikia anaesema kuwa ye ni bilionea kwenye haya maisha,
Nitamwambia kuwa hawezi nitisha,
Me ni Master Nafundisha mpaka komando kipenzi mchakamchaka,
Wanaodhania kuwa leo ntaanguka ,
Kesho nitasimama tena,
Wanaosubiri kwenye game ntapotea,
Kesho nitaonekana tena,
Ila kidonda kinauma lakini hakijawahi,
Kushiriki kulia chipsi,
Kitan bodaboda hawali chipsi,
Ila wanapakia mishikaki,
Nasikia siku hizi moto wa shule unaunguza wapita njia
Mpaka walioko shuleni,
Me ndo yule mr.face ninae facebook ya mitandao ya kijamii,
Yaani nina mawazo mengi kama vile nimewasha data za ubongo,
Karb hapa ili nikupe madini,(konk)
Ndo vile huwezi kujificha chini ya kivuli chako,
Ili kuona nani anayekuja anaekuja nyuma yako,
Tambua, unaweza ukawa mwema lakini kwa wajinga ukawa mpumbavu,
Ukiona mtu anapenda kuwashwa ujue kashafuga kucha ndefu,
Kama wakunaji wa upele yaani willy paul na Nandy kwenye game,
Ety siku hizi vipaji havikai,
Au ndo vile ng'ombe wa maskini hazai,
Siamini,
Kama huna hela usitaman mjengo,
Weka malengo huwezi jua
Wakati unawaza kupunguza mapengo,
Wenzako ndo kabisaa utawakuta wanajenga majengo,
Sokoni
Maisha ni malengo na vitengo,
Haitoshi mipango,
Elewa kuwa mipango sio matumizi,
Hivi wanaosikia baridi maskio yao ndio ngozi,
Ya kuhisi baridi,
Ama wanaoishi mkuyuni ndo wanapata kivuli halisi,
Kuliko wanaoishi chini ya jua,
Kama nanyosha upepo kila kitu kinapepea angani,
Ukipenda vya Kitonga lazima uchote maji,
Maana kazi isio kuwa na mtaji duniani ni kuuza mwili,
Mtaani wanasema shule ndo inakuweka kwenye map,
Wakati siku hizi degree ni kipima joto,
Aise kuna watu wanachekesha hadi kope zao ni kicheko,radio fm
Unaambiwa mjini shule
Kama ujaenda shule
Akili yako ndio mali pia madini,
Siku hizi mambo ya leo ni mengi,
Mpaka mambo ya jana ni msingi,
Mambo yanasonga lakini hayawezi kusonga mistari,
Kama songa mc kila kona ma-mc kibao,
Mpaka maarusi wanaona jauh kwenye arusi na kuogopa kufunga ndoa,ndoa isije ikawa ndoano,
Maisha ya bongo yanaudhi na sindano,
Ukiyazingua yanakushona kwa nyuzi,
C unajua pesa ina majina yake siku hizi,
Kwahyo usishangae pesa ya kutumika kwako ukiwa haupo tayari,
Kuishika wala kuiona ikawa rambirambi ukiwa haupo tena duniani,
IT'S OVER
NI KAZI KUPATA KAZ
KAMA HUNA KAZ
ULIE NA KAZ
ACHA USELA KWENYE KAZ
UTAK KAZ
ACHA KAZ
UKAE BILA KAZ
UONE ILIVYO KAZ
KUKAA BILA KAZ