Eleza Lyrics
- Genre:Pop
- Year of Release:2020
Lyrics
CHORUS
Una shida na jirani yako
eleza Mama, eleza baba
Una furaha na mpenzi wako
eleza Baba, eleza mama
VERSE 1
Kwenye maelezo yako
kuna uponyaji; wa simanzi na huzuni
Kwenye maelezo
kuna uumbaji wa furaha maishani
Jieleze, eleza mama
jieleze, Eleza
Jielezeee, eleza baba
jieleze, eleza..
CHORUS
Una shida na jirani yako
eleza Mama, eleza baba
Una furaha na mpenzi wako
eleza Baba, eleza mama
VERSE 2
Ni muhimu ujue, hali ya mpokeaji
kabla hujasema lolote
Jema au baya, unavyo lifikisha yaweza kujenga au bomoa
Ukali na upole, vina sehemu yake
angalia iwe sahihi
na hayo mazingira, ndiyo yanayo pelekea mahusiano mazuri
BRIDGE
Eleza eleza, eleza we' eleza
INTERLUDE
Unajua inafika mahali
kuna vitu una tamani kuzungumza
lakini huwezi kumweleza ndugu, rafiki jirani na hata jamaa wako wa karibu
kumbuka Mungu, Baba Muumba Mbingu na Nchi, yeye aliye juu, yupo hai
Na neno lake linasema unikumbushe, tuhojiane.
Eleza mambo yako upate pewa haki yako
Mueleze Mungu...
CHORUS
Una shida na jirani yako
eleza Mama, eleza baba
Una furaha na mpenzi wako
eleza Baba, eleza mama